Habari

Hatimaye Besigye apewa dhamana na Mahakama Kuu nchini Uganda

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye, ambaye amezuiliwa kwa wiki kadha, amepewa dhamana na Mahakama Kuu nchini humo.

160615111409_besigye_court_512x288_bbc_nocredit

Jaji Wilson Masalu Musene amempa kiongozi huyo wa chama cha Forum for Democratic Change dhamana ya dola 30,000 za Marekani.

Jaji amemwamuru Dkt Besigye kutojihusisha na vitendo vya kuzua ghasia na adumishe amani katika jamii hadi kesi ya uhaini inayomkabili isikizwe na uamuzi kutolewa.

Ametakiwa awe akifika kortini mara moja kila wiki mbili kuanzia Julai 26.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, wafuasi wa Beisgye wameimba wimbo wa taifa wa Uganda na kushangilia baada ya kiongozi wao kupewa dhamana.

Besigye amerejeshwa selo kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kumwachilia huru kwa dhamana hiyo.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents