Habari

Hatimaye Dkt. Mollel na Mtulia waapishwa Bungeni

Naibu Spika, Tulia Ackson, leo Aprili 3, 2018 amewaapisha wabunge wawili, Dk Godwin Mollel na Maulid Mtulia.

Godwin Mollel wa Siha na Maulid Mtulia wa Kinondoni wameapishwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo yao baaada ya wao wenyewe kuhama vyama vyao vya awali na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Utukumbuka Mtulia alikuwa mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi (CUF), wakati Dkt. Mollel alikuwa mbuge wa Siha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Baada ya wote wawili kuhamia CCM waliteuliwa na chama hicho kuwania tena nafasi hiyo ambapo walifanikiwa kushinda kwa mara nyingine tena katika matokeo yaliyotangaza February 18, 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents