Habari

Hatimaye familia ya kifalme Uingereza yapata mtoto wa kiume

Tarehe (22 July, 2013) imeingia katika historia ya familia ya kifalme nchini Uingereza baada ya mke wa mjukuu wa mfalme wa Uingereza Prince William, Kate Middleton kujifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya St.Mary’s, Paddington Mashariki mwa mji wa London.

uk2

Mtoto huyo wa kifalme alizaliwa majira ya saa kumi na dakika ishirini na nne jioni saa za Uingereza huku baba yake Prince William akishuhudia.
Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto huyo limetolewa na kuwekwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu la kifalme la Uingereza la Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza zilivyo.

uk3

Taarifa rasmi iliyosainiwa na jopo la madaktari bingwa kuthibitisha kujifungua kwa Duchess wa Cambridge ilipelekwa kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa polisi.

Baada ya taarifa hizo zilizokuwa zikisubiriwa kwa hamu kutangazwa, Shangwe na vifijo vilitanda huko Uingereza na watu walionekana kumiminika kwa wingi wakielekea katika kasri ya kifalme kutaka kupata taarifa zaidi.

Tazama picha za tukio hilo

uk4

uk5

uk6

uk7

uk9

uk10

uk11

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents