Hatimaye Kevin Gates aachiwa huru

Rapa wa marekani Kevin Gates hatimaye katoka gerezani baada ya kutumikia miezi tisa kwa kosa la kumiliki silaha kali.

Jana Jumatano asubuhi alitoka gerezani la jimbo la Illinois ambapo alikuwa akitumikia miezi 9 ya hukumu yake ya miezi 30.

Kumbuka kwamba Gates awali alikuwa na hatia na kuhukumiwa miezi 5 gerezani kwa kumpiga shabiki wa kike katika kifua wakati wa show yake moja mwaka 2015. Hata hivyo, siku alipokuwa anatakiwa kutoka gerezani, hati miliki iliyohusiana na silaha ilipatikana na alirudishwa gerezani kwa hukumu ya miezi 30.

Rapa huyo wa New Orleans atakuwa chini ya usimamizi wa lazima na hapaswi kumiliki silaha yoyote.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW