Habari

Hatimaye Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Spika wa bung la Zimbabwe ametangaza rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe amejiuzulu nafasi ya urais aliyoishikilia kwa miaka 37.

Robert Mugabe

Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo lililotolewa muda mfupi uliopita huku  mchakato wa kumuondoa madarakani rais huyo kupitia Bunge ukiwa umesitishwa.

Kupitia ukurasa wa rasmi wa Twitter wa Chama tawala nchini humo cha Zanu-PF kimethibitisha taarifa hizo kwa kuandika “R G Mugabe amejiuzulu. Safari ya zama mpya inaanza rasmi”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents