Habari

Hatimaye Rais Trump afanya mazungumzo ya siri na hasimu wake Kim Jong Un

Baada ya kutumiana vijembe na maneno ya kashfa kwa muda mrefu kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, hatimaye wawili hao wafanya mazungumzo mafupi kwa siri wiki mbili zilizopita.

Rais Donald Trump na Kim Jong Un

Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya  Mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini Marekani (CIA), Mike Pompeo wikiendi ya pasaka kuzuru mjini Pyongyang na kufanya mkutano wa siri na kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong Un,  hii ni kwa mujibu wa duru za vyombo vya habari nchini Marekani.

Mkutano huo ulifanyika kwa lengo la maandalizi ya mkutano mwengine mkubwa kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong Un ambapo hadi sasa bado haijajulikana ni wapi utafanyika.

Hata hivyo, Rais Trump amekiri kufanyika kwa mazungumzo na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kwa njia ya simu, wakati wa sherehe za kumpokea Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe zilizofanyika mjini Florida juzi Jumatatu.

Mkutano huo wa siri ambao haukutarajiwa ndio utakuwa mkutano wa kwanza mkubwa  kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000, wakati Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani kipindi hicho, Madeleine Albright alipokutana na Kim Jong-il, babake kiongozi wa sasa wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents