Michezo

Hatimaye Wayne Rooney asaini mkataba mpya na Man United, atalipwa £300,000 kwa wiki

Wayne Rooney jana usiku amemshukuru kocha wake David Moyes baada ya kujihakikishia mustakabali wake katika klabu ya Manchester United, kufuatia kusaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomnfanya apate mshahara wa £300,000 kwa wiki.

Rooney
Rooney amethibitisha kusaini kwake mkataba mpya United kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema ‘furaha sana’

Awali Rooney alikuwa amepa nga kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kutofautiana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson. Mabingwa hao wa ligi Kuu ya England walilazimika kupambana na ofa ya dau la £ milioni 30 kutoka Chelsea

Moyes alisimulia jana namna ambavyo alimshawishi mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kubaki Old Trafforf alipokutana naye katika kikao chake cha siri kilichofanyika Juni mwaka jana. Naye Rooney ametoa shukrani zake kwa kocha wake huyo baada ya kusaini mkataba utakaomalizika Juni mwaka 2019. Mkataba huo unamfanya Rooney awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani.

Moyes na Roney
Wa hapa hapa: Rooney (katikati) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Ed Woodward na kocha David Moyes jana baada ya kusaini mkataba mpya

MALIPO MAPYA YA ROONEY

Pauni 15,600,000 kwa mwaka
Pauni 300,000 kwa wiki
Pauni 43,000 kwa siku
Pauni 1,800 kwa saa
Pauni 30 kwa dakika
50p kwa sekunde

CHANZO: DAILY MAIL

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents