Michezo

Hatma ya Argentina ipo mikononi mwa Waafrika,Diego Maradona aitisha kikao cha dharura na wachezaji

Gwiji wa soka raia wa Argentina, Diego Maradona ameomba kikao na wachezaji wa timu yake ya taifa kabla kutupa karata yao ya mwisho kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi ya Nigeria ‘Super Eagles’ ili kujua hatma yao ya kusonga mbele.

Gwiji wa soka raia wa Argentina, Diego Maradona

Timu ya taifa ya Argentina ipo kwenye hali tete ya kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kufungwa mchezo mmoja dhidi ya Croatia na sare moja na Iceland huku ikisaliwa na mechi moja pekee mbele ya Waafrika Nigeria siku ya Jumanne ya wiki hii jambo ambalo limemfanya nguli wa soka duniani, Maradona kuomba kikao na wachezaji wake akiwemo Lionel Messi ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wao ujao.

Argentina ambayo ipo kwenye kundi D inahitaji pointi tatu kutoka kwa Waafrika Nigeria ili kuweza kuingia hatua ya 16 bora na sare yoyote haitomsaidia kwakuwa vijana hao wa ‘Super Eagles’ tayari wana alama tatu kibindoni wakishika nafasi ya pili wakati ya kwanza ikichukuliwa na Croatia wenye ponti sita na Iceland ikiburuza mkia.

Akizungumza na vyombo vya habari, Maradona amemtupia lawama rais wa chama cha soka nchini Argentina, Claudio Tapia huku akisisitiza kuwa ilipofikia timu hiyo kwa sasa inauma mno.

Maradona is “furious and upset” and criticised Argentine Football Association president Claudio Tapia.

“Inauma sana tena sana ilitugharimu sana mpaka kama taifa kufika hapo tulipo kwenye ramani ya soka alafu timu kama Croatia inakuja kutufunga tena kwa magoli matatu ikituacha bila hata kunga bao hata moja,” amesema Maradona.

Maradona ambaye  ni mshindi wa tuzo ya Golden Ball akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina kombe la dunia la mwaka 1986 amesema anahitaji kukutana na kocha Jorge Sampaoli pamoja na wachezaji angalau kujadiliana kwa muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents