Michezo

Hatma ya Simba mikononi kwa URA

Kikosi cha klabu ya Simba hii leo kitaingia Uwanjani kutupa karata yake dhidi ya timu ya URA katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar kuwania nafasi ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Simba SC ambayo ipo nafasi ya tatu ya kundi A ikiwa na pointi nne, itahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mchezo wa mwisho klabu hiyo ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wanaramba ramba timu ya Azam FC ambayo imeshatinga hatua hiyo kwa kuwa na jumla ya pointi 9 baada ya kucheza mechi nne huku ikiongoza kundi hilo.

Vita vikali hii leo ni kati ya wakusanya kodi wa Uganda , URA ambayo ipo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya pointi saba dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu wakati timu za Mwenge na Jamhuri zikiwa zimesha toka katika mbio kinyang’anyiro cha Kombe la Mapinduzi.

Kwa matokeo yoyote yale yataifanya Simba SC kuyaaga mashindano hayo ya Mapinduzi Cup kwa mwaka huu na kuwa ni mashindano ya pili kupoteza baada ya yale ya FA.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents