Habari

Hatua inazochukua serikali kukabiliana na kushindwa kesi Mahakamani

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema ili kukabiliana na tatizo la kushindwa kwa baadhi ya kesi Mahakamani itahakikisha kuwa mashahidi muhimu wanapatikana na kuwaandaa ipasavyo mashahidi kabla ya kutoa ushahidi.

Akijibu kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria,leo Bungeni mjini Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde ambapo alisema ni kujiandaa vyema katika kila shauri kuwajengea uwezo mawakili wa serikali ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

“Katika kukabiliana na changamoto hizo serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa ikiwemo kuhakikisha kuwa mashahidi muhimu wanapatikana kuwaanda ipasavyo mashahidi kabla ya kutoa ushahidi, kujiandaa vyema katika kila shauri kuwajengea uwezo mawakili wa serikali ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na ipasavyo kushirikiana na vyombo vya upelelezi kama vile Takukuru na jeshi la polisi,” alisema Mavunde.

“Katika maeneo ambayo yanasababishwa kuwa hafifu na kurekebisha kasoro hizo, kukata rufaa na kuendelea kuzishauri taasisi za serikali kutoa taarifa mapema kwa mwanasheria mkuu wa serikali, katika kila shauri lililofunguliwa Mahakamani ili kwa pamoja kuangalia namna ya kulinda maslahi ya serikali katika shauri husika.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents