Habari

Hatua za wabunge Lema na Nassari kuelekea TAKUKURU ilianza hivi (Video)

Safari ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ya kuelekea TAKUKURU ilianza September 27 mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Takukuru , Valentino Mlowola kuwaruhusu kupeleka ushahidi wa tuhuma za rushwa kwa madiwani waliokihama chama hicho na kuhamia CCM kwa madai ya kupewa rushwa.

Wabunge hao Lema na Nassari walianza kuelekea TAKUKURU kutoa ushahidi kuhusu madiwani 7 waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.

Wabunge Lema na Nassari kuunguruma Takukuru

Baada ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, Mlowola kuwaruhusu kupeleka ushahidi huo,Oktoba 2 mwaka huu waliwasili katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es salaam kupeleka ushahidi wa awali wa wabunge wa chadema kudaiwa kununuliwa. Ambapo katika kuwasili huko waliongozana na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ambaye alisema kuwa hata jimboni kwake madiwani walinunuliwa hivyo na yeye atakuwa ni mmoja ya watu watakao fungua jalada TAKUKURU.

Hata hivyo siku ya kwanza walipofikisha ushahidi wa awali ulipokelewa na walieleza kuwa wamepokelewa na walikubaliana mambo ya msingi ambayo hawakuyaleta bayana, ambapo Mhe. Nassari kesho yake aliambiwa awasili tena katika Taasisi hiyo kwaajili ya kufungua jalada.

Video: Wabunge Lema na Nassari watinga TAKUKURU Dar kuishtaki CCM

Siku hiyo ilipofika Bongo5 ilimtafuta Mbunge huyo wa Arumeru alisema kuwa siku hiyo hatawasili katika taasisi hiyo hivyo kuna ushahidi anausubiri kutoka Arusha ili awasili katika ofisi hizo.

Video: Nimeingia TAKUKURU kijasusi nimetoka kijasusi – Joshua Nassari

Oktoba 4 mwaka huu, Mbunge Nassari aliwasili Takukuru kwaajili ya kuwasilisha ushahidi wa awamu ya pili wa tuhuma zinazo wahusu madiwani wanane waliohama CHADEMA na kujiunga na CCM katika baadhi ya kata Mkoani Arusha.

Mh. Nassari akiingia ofisini hapo alionekana akiwa ameshika ‘Flash’ na ‘Hard Disk’ ambavyo pia amedai vifaa hivyo alibebea ushahidi wa kutosha.

Mbunge huyo alidai kuwa usalama wa maisha yake uko mashakani kulingana na jumbe za vitisho anazopokea baada ya kufichua sakata hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents