Habari

Hatua zitachukuliwa kwa atakae vuruga amani – Waziri Mkuu

By  | 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ametoa kauli hiyo Jumatano hii, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam.

“Nataka niwahakikishie wageni wote waheshimiwa Mabalozi kwamba Tanzania ipo imara, Tanzania bado ipo salama na bado ni Watanzania wa amani na umoja na utulivu .Tutachukua hatua madhubuti kwa atakae kuja au kutoka popote atakae jaribu kuvuruga amani yetu ya Tanzania, alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments