Michezo

Hatuendi Bernabeu kumshanga Ronaldo – Pochettino

Meneja wa klabu ya Tottenham Hospur, Mauricio Pochettino amewataka wachezaji wake kuacha kujipanga kumkabili Cristiano Ronaldo na badala yake kujiandaa kupambana na Real Madrid.

Meneja wa klabu ya Tottenham Hospur, Mauricio Pochettino

Pochettino ameyasema hayo leo wakati wakijiandaa na safari yao ya kuelekea katika dimba la Santiago Bernabeu nchini Hispania kwenye mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya ‘UEFA’ utakao pigwa hapo kesho siku ya Jumanne dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid.

Wachezaji wa Spurs watakutana na Ronaldo ambaye amerejea katika kiwango chake baada ya ya kuisaidia klabu yake kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Getafe katika ligi ya La Liga siku ya Jumamosi.

Mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo 

Baada ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Bournemouth siku ya Jumamosi, Pochettino amesema Ronaldo ni mchezaji muhimu lakini wanawachezaji wengi wazuri.

“Wana kikosi kizuri na wana kocha bora, klabu bora lakini unahitaji umoja ili uweze kushinda ubingwa,” amesema Pochettino.

“Cristiano ni kama Lionel Messi ana athari yake anapokuwepo ndani ya timu ni mchezaji bora wa dunia.”

“Ni vigumu sana kusema kitu kingine chochote kwa wachezaji hawa ni kama Diego Maradona kwa namna walivyo. Wanauwezo wa kubadili mchezo na kuisaidia timu yake kupata matokeo, hatuchezi na Real Madrid bali na wachezaji bora kabisa duniani.”Amemalizia kocha huyo wa Spurs.

Tottenham ilianza kuchanga karata zake katika kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya msimu huu baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya   Borussia Dortmund na kutoka na ushindi ugenini wa mabao 3-0  mbele ya Cypriots APOEL Nicosia.

Wakati kwa upande wa Real wenyewe wakianza na ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya  APOEL nyumbani na 3-1 ugenini dhidi ya Dortmund wakiwa wanatetea taji lao chini ya kocha Zinedine Zidane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents