DStv Inogilee!

Hatukuwekwa mbaroni Athens!!!

Siku moja baada ya kuripotiwa na DHW kuwa wasanii Ray C na TID walikwama kwenye kiwanja cha Athens,Ugiriki kutokana na kutaka kuingia nchini humo kinyume cha sheria,…… tuliwaahidi kulifwatilia sakata hilo kwa karibu na kwa bahati nzuri tulifanikiwa kumpata mwanadada Ray C moja kwa moja na haya ndiyo machache aliyokuwa nayo ya kusema.

Ray C (kushoto)kwenye picha ya pamoja na TID wakiwa Berlin,German.

DHW:Habari ya kazi dada

RAY C: Aisee siyo mbaya baridi tu huku mtu wangu hahahaha

DHW:Sasaaaa kuna tuhuma huku kuwa wewe na TID mlishikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Athens na kulikuwa na taarifa kuwa mngefunguliwa mashtaka au kulipishwa fine kutokana na kuingia nchini humo kinyume cha sheria??????

RAY C:Noo sio kihivyo kilichotokea ni kwa tulitakiwa kufanya show last week Athens yaani Jumamosi…..so tukaondoka hapa Germany ijumaa ndege tulioondoka nayo haikuwa ya moja kwa moja kutoka hapa berlin kwenda athens,kwahiyo promota wetu alituchukulia ndege ya shirika la Czech Republic (Czech Airline),so tulipanda hiyo ndege lakini haikwenda moja kwa moja ilikuwa inapitie nchi nyingine for 2 hours then inatua athens,hapo prague tulikuwa transit for 2 hours then tukachukua nyingina mpka Athens.

DHW:ehe endelea baada ya kufika Athens ikawaje?

RAY C:Sasa kilichotokea ni kwamba aliyetukatia ticket hakutuambia kwamba Prague ni nje ya Shenghen,na visa zetu sisi ni za kuzunguka hapa hapa nchi za Scandinavia,so prague iko nje,sasa tulipofika athens tukaambia kwamba visa zetu zimeshaisha hatuwezi kuingia mpaka tu renew visa,tulichokifanya tukawaambia pale uwanja wa ndege kuwa weny makosa sio sisi ni wale waliokata ticket!!!! coz sisi tulipita Prague kama transit yaani tlikuwa pale pale Airport.

DHW:Kwahiyo ni kweli kuwa mlishikiliwa na kuhojiwa?

RAY C:Hapana hatukuhojiwa na mtu mwingine yoyote zaidi ya meneja wa hiyo ndege pale Athens,na hatukutoka hata nje ya airport,wakapiga kwenye hilo shirika la ndege wakakubaliana na ndipo tukapaswa kurudi tena Germany ili watuongezee muda wa Visa….na tulipofika wakatugongea Visa nyingine coz ilikuwa ni makosa yao.

DHW:Kwa hiyo hiyo kule mlikotoka hamkupigwa fine yoyote?

RAY C:Hapana hatukuchukuliwa hata shilingi moja!!!….coz makosa walifanya wao kampuni ya ndege….coz wangetuambia mapema kwamba visa zetu haziruhusiwi kupita Prague tungechukua ndege nyingine….na kingine ni kwamba kama ingekuwa ni kosa letu basi tusingepewa visa nyingine tungerudishwa Tz mara moja.

Kama tulivyowaahidi wasomaji wetu kuwa tungefanya njia yoyote kuhakikisha mnaoufahamu ukweli wa tukio hilo……..na kama utakuwa umefwatilia kwa makini mazungumzo hayo hapo juu….basi bila shaka utakuwa umeelewa mwenyewe kilichotokea.

Kwa mujibu wa Ray C, Jumamosi hii watakuwa Sweden…na wale wa Athens basi wategemee kuwaona wanamuziki hao maarufu kutoka Bongo tarehe 15 mwezi huu.

Source: Darhotwire

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW