Burudani

Hatumtaki: Mashabiki waponda Ben Affleck kuigiza kama Batman

Ben Affleck ameteuliwa kuigiza kama Batman kwenye muendelezo wa Man of Steel. Kwenye filamu hiyo, Ben Affleck akiwa Batman atakutana kwa mara ya kwanza na Henry Cavill atakayeigiza kama Superman.

i.0.ben-affleck-batman

Hata hivyo, mashabiki wameuponda uamuzi huo na kumuona Ben hafai kabisa kuwa Batman. Sekunde chache baada ya Affleck kutangaza, mashabiki wa kitabu cha Batman wameanzisha timbwili huku mitandao ya kijamii ikifurika ujumbe wa kuponda.

Wengine wamemuomba mpaka Rais Barack Obama aingilie kati suala hilo ili muigizaji huyo asipewe uhusika wa Batman.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents