Habari

Tunataka mabadiliko – Raila Odinga

Umoja wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya NASA, umedai kutaka mabadiliko yafanyike ndani ya Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais.

Raila Odinga

Kiongozi wa umoja huo wa upinzani, Raila Odinga, amesema Tume ya Uchaguzi haiaminiki na haiwezi kusimamia Uchaguzi utakaokuwa huru na haki kama Mahakama Kuu ilivyoagiza.

Kauli ya Odinga imekuja baada ya kuanza kwa kampeni yake ya kwanza jijini Nairobi leo kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Juu Ijumaa iliyopita ambapo ilibatilisha matokeo ya ushindi wa Uhuru Kenyatta .

Pamoja na hayo Odinga amekosoa kauli ya Rais Kenyatta ya kuwashtumu Majaji kwa kudai kuwa upinzani hawataki uchaguzi lakini wanataka serikali ya muungano, madai ambayo Odinga amepuuzilia mbali na kusema hawawezi kushirikiana na wezi wa kura.

SOMA ZAIDI – Rais Uhuru Kenyatta aonywa na Chama cha Mawakili nchini Kenya

Kenya inaelekea kwenye Uchaguzi mpya ndani ya siku 60 baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kwa kubaini kuwa, haukuwa wa huru na haki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents