Michezo

Hatuna Udada na Ukaka sisi kama Singida United na klabu ya Yanga bali tuliwasaidia tu wachezaji – Sanga

Hatuna Udada na Ukaka sisi kama Singida United na klabu ya Yanga bali tuliwasaidia tu wachezaji - Sanga

Mkurugenzi wa klabu ya Singida United kutoka mkoa Singida Festo Sanga amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na yale maneno yanayoendelea kuzagaa mtandaoni kuwa klabu yao inaukaribu sana na klabu ya Yanga.

Sanga ameonea haya katika mkutano alioufanya na waandishi,mkutano huo ulifanyika jana katika tukio la kumtambulisha mdhamini wao mpya ambaye ni Sports Master,hii ni kampuni ya Kitanzania ambayo itahusika katika kuitengenezea klabu hiyo vifaa vya michezo ikiwemo Jezi viatua pamoja na vifaa vingine vyote vya kimichezo.

Baada ya tukio hilo kumalizika ulifuata muda wa maswali na miongoni mwa Waandishi aliuliza swali linalohusiana na ukaribu wao na klabu ya Yanga kwani ilifikia mpaka hatua wanaazimishana  Wachezaji Sanga alijibu:-

“Haya maneno yapo kweli na tumeyasikia ila sisi kama Singida United tunatoa tamko rasmi leo kuwa hatuna undugu wowote wala Ukaka na Udada na klabu ya Yanga inshu za kubadilisha wachezaji ni kwa sababu rais wa klabu yetu Mh:Mwigulu Nchemba ni shabiki wa Yanga na sisi ili kuonyesha hatuna Undugu nao ndio maana katika michezo yote ya msimu uliopita hata katika michuano ya Azam Confederetion tuliifunga Yanga karibia michezo yote.”

Klabu ya Singida United ilipanda daraja mwaka jana na kufanikiwa kufanya vizuri katika ligi kuu nchini Tanzania bara kwa kushika nafasi ya tano na hata katika baadhi ya michuano mfano michuano ya FA ilifanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo.

 

By Ally Juma.

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents