Habari

Hatutaki siasa katika mambo ya msingi – Mhe. Mhagama

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama amewaonya watumishi wa Serikali wanaokwamisha mipango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya kuingia katika uchumi wa viwanda akisisitiza kuwa, hawatavumiliwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema hayo juzi wakati akifunga semina ya siku mbili ya wakurugenzi, viongozi na watendaji wengine wa mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania Bara na Visiwani ili kujadiliana na kupata mwafaka wa miradi 25 inayotaka kuanzishwa na mifuko hiyo.

“Hatutaki siasa katika mambo ya msingi na watumishi wa Serikali, wanaodiriki kuleta urasimu usiokuwa na sababu za msingi na kudiriki kukwamisha mipango hii, watatimuliwa kwani hawana nia nzuri na serikali. Sasa hakuna kulala wala kurudi nyuma alisema Muhagama ni kusonga mbele mpaka kieleweke ,” alisema Muhagama.

Akizungumzia mifuko hiyo kuwa na changamoto nyingi, Waziri alisema kwa kiasi kikubwa zinasababisha malalamiko miongoni mwa wanachama na malalamiko mengine yanahusu huduma kwa wanachama. Hata hivyo Waziri Mhagama alitoa agizo kwa wahusika wote kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo hayo kuboresha huduma kwa wanachama.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents