DStv Inogilee!

Hatutaolewa, mpaka kanisa liruhusu tuolewe kwa ndoa na mwanaume mmoja-Waongea kwa hisia mapacha waliofanana (+video)

Kama kwenye familia yako umebahati kuishi na mapacha basi utakuwa upendo uliopo baina ya watu hao, na hili limejionesha kwa wanamitindo warembo zaidi nchini Argentina, Nadinne na Dannita ambao wanataka kuolewa na mwanaume mmoja.

Wanamitindo hao ambao wamejipatia umaarufu nchini Argentina kupitia maonesho ya kimataifa ya mitindo, wamesema kuwa hawawezi kuishi mbali wameshazoeana toka utotoni na hata kuolewa wataolewa na mwanaume mmoja.

Mapacha hao ambao tayari wamefikisha miaka 30, kupitia mtandao maarufu wa brobible.com wamesema kama Kanisa Katoliki nchini humo halitaruhusu ndoa ya wanawake wawili basi hawataolewa mpaka kufa kwao.

“Hatuwezi kuishi tofauti au sehemu mbali mbali, sisi ni wamoja mpaka kufa. Tunasubiri maombi yetu kama Kanisa halitaruhusu tutaendelea kuishi kwa hivi hivi wawili bila kuolewa mpaka kufa kwetu,“wamesema wawili hao ambao wamekiri kuwa wamempata mwanaume mmoja ambaye amekubali kuwaoa.

Mapacha hao mpaka sasa, wanatumia akaunti moja za mitandao ya kijamii na wameanzisha kampuni ya mavazi na ni moja ya watu 10 wanaoingiza pesa nyingi nchini Argentina kupitia posti zao wanazoweka mitandaoni. huu ni ukurasa wao wa matangazo wa Instagram

Warembo hao wanalipwa kiasi cha dola $25,000 sawa na Tsh milioni 57 kwa wiki, hii ni kutokana na kuposti picha zao wakiwa kwenye maeneo ya Hotelini au Sehemu za kitalii kama Ibiza n.k .

Hata hivyo, warembo hao walishawahi kujitokeza na kukiri kuwa maumbo yao sio ya asili wamefanyiwa upasuaji kuongeza makalio.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW