Habari

Hatuwezi kuwa na nchi ya ‘watu wasiojulikana’ – Mhe Nape Nnauye (+video)

By  | 

Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye amesema anakerwa na kauli ya ‘Watu Wasiojulikana’ kwani ni njia moja wapo ya kuficha watu wanaofanya uhalifu nchini.

Akizungumza na Bongo5, Nape amesema hakuna watu wanaoweza kutekeleza maovu halafu wasijulikane, huku akivitaka vyombo vya habari na Wananchi kuchoma vichaka vya watu wasiojulikana kwa kuwataka wahusika wawajike kwa kuwasaka watu hao.

Hakuna watu wasiojulikana, hii ni dhana ya kufurahishana mtaani, hatuwezi kuwa na nchi ya watu wasiojulikana aaahhhh, ni watu hawataki kutimiza wajibu wao then wanajificha kwenye kichaka cha watu wasiojulikana, watu wasiojulikana ni kina nani? leo nenda mtandaoni kamtukane kiongozi halafu useme mimi sijulikani uone utakapotafutwa hadi baharini, sasa kama tuna uwezo wa kumtafuta aliyekomenti negative tunashindwaje kumtafuta aliyenyanyua silaha kumpiga mtu?,“amesema Mhe. Nape Nnauye.

 

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments