Mitindo

Hawa – Mrembo anayetamba Afrika Kusini

HawaTunaweza kuona jinsi Tanzania inavyoweza kupata mashavu ya kufa mtu katika nchi za watu kutokana na juhudi ambazo wasanii wa aina mbali mbali ikiwa ni pamoja masuala ya mitindo, muziki, michezo n.k, jambo ambalo linaashiria kuwa iwapo tutaamua kufanya jitihada zaidi, upo uwezekano nchi yetu kutambulika duniani kama nchi ya wenye vipaji

HawaTunaweza kuona jinsi Tanzania inavyoweza kupata mashavu ya kufa mtu katika nchi za watu kutokana na juhudi ambazo wasanii wa aina mbali mbali ikiwa ni pamoja masuala ya mitindo, muziki, michezo n.k, jambo ambalo linaashiria kuwa iwapo tutaamua kufanya jitihada zaidi, upo uwezekano nchi yetu kutambulika duniani kama nchi ya wenye vipaji.

 

 

 

Hawa AbdulQadir (22) toto la kisomali linalofanya mitkasi zake nchini Afrika kusini kama mwanamitindo wa kulipwa ambaye alizaliwa na kukulia hapa bongo katika Wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma, akasoma elimu yake ya msingi katika shule ya Mtajeta iliyopo hapo hapo wilayani akajiunga na shule ya kiislamu ya Kunduchi Girlz ya hapa bongo na kwenda umalizia elimu yake ya sekondari mkoani Tanga katika shule ya Popatlal.

 

 

 

Hakuaishia hapo mtoto alitia timu jijini na kupiaga kozi tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na mafunzo ya Lugha ya Kingereza pale British Council na masuala ya Secretary.

 

 

 

“kusema Kweli kabisa Miriam Odemba ndiye aliyeniingiza katika masuala ya uanamitindo ambapo alinikutanisha na Moustapha Hasanali 2003 ambapo niliweza kushiriki katika fashion show yake nikatokea kumvutia Lucy Kihwele ambaye alinitaka nishiriki katika kinyang’anyiro cha kumsaka ‘Face Of Afrca’”

 

 

 

Aliendelea kusema “walijitokeza jumla ya washiriki 250 wakachijwa na kubaki 6 na mimi nikiwa mmoja kati ya hao, mchujo ukapita tena tukabaki wawili na mimi nikachaguliwa kuiwakilisha Bongo katika Face Of Afrika ambapo alikwenda nchini Zambia ambapo zilifanyika nusu fainali lakini hakufanikiwa kushinda kwenda fainali isipokuwa washkaji zangu pamoja na mshindi wakanipa mchongo mpaka sasa nakamua bondeni.

 

 

 

Yote haya binti aliyafanya pasi na kuwashirikiha wazazi wake ambao wasingeweza kukubali kabisa mtoto wao ashiriki katika masuala hayo kutokana na imani ya kidini waliyo hayo katika familia yao “baadae washua walikuja wakaona kwenye magazeti ambayo yaliandika habari zangu sipendi kuelezea walireact vipi na ndio maana katika interviews sipendi kulizungumzia hilo” alisema Hawa.

 

 

 

Ukimtazama hutakuwa na la kubisha kuhusiana na muonekano alio nao mtoto huyu mwenye asili ya kisomali lakini ni mzaliwa wa bongo, rangi nyeusi ya ukweli kabisa isiyojuana na na vipodozi, nywele ndefu ya asili, figa ya kimodo ambayo inamfanya anakuwa na kila sababu ya kufanya vizuri katika michongo hiyo Ama kweli ni haki yake jamani kula mashavu hayo pande za bondeni.

 

 

 

Ameingia mkataba na kampuni ya STAR Agency iliyopo jiji Johannesburg nchini Afrika kusini ambayo imemuweka katika Agency ya Outlaws iliyopo Cape Town “naenjoy sana kufanya kazi yangu kwani nimeipata kwa jitihada zangu, na nilichogundua kweli watanzania ambao huenda nchini Afrika Kusini katika masuala ya Modeling wakirudi huwadanganya wenzao kwa kudai kule ni pagumu kupata michongo jambo ambalo si kweli kama kweli unafanya jitihada lazima unapata pakujiweka kwani kazi zipo ukikosa hapa ukijaribu pale waweza pata”

 

 

 

Amewataka wabongo wajitokeze na kwenda kujaribu bahati yao kule kwani anaamini kuna watu wana vigezo vya kufanya kazi kule sema roho mbaya za watu waiopenda maendeleo ya wenzao ndizo zinazowakatisha tama na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

 

 

 

“kazi ninayofanya kwa huku nimeridhika nayo kabisa kwani si kama nio kwenye Agency tu nasubiri kazi, ‘NO’ kazi za kumwaga na namshukuru mungu Napata kazi mara kwa mara, hii inamaanisha Napata fedha pia, vitu kama ofa kutoka kwenye maduka na makampuni mbali mbali ni vya kawaida sana hasa ukizingatia nimejitangaza na kukubalika vya kutosha”-Hawa.

 

 

 

Malengo aaliyonayo Bi Hawa “kwa kuwa nimesomea masuala ya biashara natarajia kuuza bihaa zangu mwenyewe ikiwa ni pamoja na mavazi, viatu, mabegi n.k vyote vikiwa na nembo yangu na Inshaallah naamini mungu atanisaidia kuyatimiza malengo yangu” alimaliza Hawa AbdulQadir.

 

 

 

Bofya hapa kupata ujumbe mfupi kutoka kwa Hawa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents