Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hawa ndio wachezaji 10 wanaokumbukwa kwa kufunga hatrick ligi kuu Uingereza, Waafrika wapo wawili

Unafahamu wachezaji ambao wamewahi kufunga hatrick katika ligi kuu ya Uingereza ambao hawawezi kusahaulika katika historia ya ligi hiyo? Kuna wachezaji takriban 50 ambao wamewahi kufunga hatrick katika ligi hiyo. Wafahamu wachezaji 10 hapa chini waliowahi kufanya hivyo.

Dimitar Berbatov (Manchester United 3-2 Liverpool) — September 19, 2010

Ukiambiwa umtaje mchezaji ambaye amewahi kuifunga hatrick klabu ya Liverpool hutaacha kumtaja Dimitar Berbatov. Mchezaji huyo alifanya balaa hilo katika uwanja wa Old Traford September 19, 2010.

Katika mchezo huo Man United iliibuka na ushindi wa mabao 3-2. Berbatov alifunga mabao hayo dakika ya 42, 59 na 84.

Nwankwo Kanu (Chelsea 2-3 Arsenal) — Oktoba 23, 1999

Nwankwo Kanu ni miongoni mwa wachezaji kutoka Afrika ambao wanakumbukwa sana katika ligi kuu ya Uingereza kwa kufunga hatrick. Mchezaji huyo wa zamani wa Nigeria alifanya hivyo wakati akicheza Arsenal Oktoba 23, 1999 dhidi ya Chelsea.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, Kanu alifunga hatrick hiyo kwenye dakika ya 75, 83 na 90.

Sadio Mane (Southampton 6-1 Aston Villa) — May 16, 2015

Sadio Mane ni mchezaji mwingine kutoka Afrika ambao watakumbukwa sana kwa kufunga hatrick. Mchezaji huyo aliwahi kufanya hivyo wakati akichezea Southampton, May 16, 2015 walipokutana na Aston Villa.

Mane aweka rekodi hiyo kwa kufunga hatrick hiyo ndani ya dakika nne. Magoli hayo alifunga katika dakika ya 13, 14 na 16.

Robbie Fowler (Liverpool 3-0 Arsenal) — August 28, 1994

Fowler ni mfungaji wa muda wote wa Liverpool na pia anashika nafasi ya sita kwa wafungaji bora wa muda wote katika ligi kuu ya Uingerea. Miongoni mwa magoli yake yanayokumbukwa ni hatrick ambayo aliifunga August 28 ya 1994 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa ligi kuu.

Mshambuliaji huyo aliifungia Liverpool magoli hayo dakika ya 26, 29 na 31.

Luis Suarez (Liverpool 5-1 Norwich City) — December 4, 2013

Ukimtaja Luis Suarez kwa mashabiki wa Norwich City wanakumbuka mchezo ambao ulifanyika Disemba 4 ya mwaka 2013. Katika mchezo huo uliomaliika kwa mabao 5-1, ulimshuhudia Suarez akifunga hatrick ya mabao 4.

Mabao hayo aliyafunga dakika ya 15, 29, 34 na 74.

Dennis Bergkamp (Leicester City 3-3 Arsenal) — August 27, 1997

Bergkamp anakumbukwa kwa kufunga katika ligi kuu ya Uingereza kwa kufunga hatrick dhidi ya Leicester City, August 27, 1997. Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Uholanzi alifunga mabao hayo kunako dakika ya 39, 61 na 90.

Robin van Persie (Manchester United 3-0 Aston Villa) — April 22, 2013

Robin van Persie ni miongoni mwa washambuliaji ambao wamewahi kufunga hatrick zinazokumbukwa katika mchezo wa soka hasa katika ligi kuu ya Uingereza. Magoli hayo alifunga katika dakika ya 2, 13 na 33.

Alan Shearer (Newcastle United 4-3 Leicester City) — February 2, 1997

Miongoni mwa hatrick za Alan Shearer zinazokumbukwa ili pale alipoifunga Leicester City February 2, 1997.

Shearer alifunga mabao hayo kwenye dakika ya 77, 83 na 90.

Matt Le Tissier (Norwich City 4-5 SOUTHAMPTON) — April 9, 1994

Moja kati ya mechi zinazokumbukwa sana katika ligi kuu ya Uingereza ilikuwa kati ya Norwich City dhidi ya SouthHampton ambayo ilichezeshwa na refaKeith A Cooper katika uwanja wa Carrow Road.

Katika mchezo huo kiungo huyo mshambuliaji Matt Le Tissier alifunga hatrick. Magoli hayo alifunga kwenye dakika ya 57, dakika ya 63 kwa njia ya penalti na dakika ya 72.

Fabrizio Ravanelli (Middlesbrough 3-3 Liverpool) — August 17, 1996

Katika mechi hiyo ambayo ilichezwa katika uwanja wa Riverside, mshambuliaji huyo wa Italia ambaye aliichezea Middlesbrough kwa msimu mmoja akitokea Juventus, alifunga mabao hayo katika dakika ya 26 kwa njia ya penalti, dakika ya 36 na dakika ya 81.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Bjornebye (4), Barnes (29), Fowler (65).

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW