Michezo

Hawa ndio wachezaji 24 wa Taifa Stars waliochaguliwa kucheza na Benin

Leo Jumanne kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitacheza na timu ya taifa ya Benin Novemba 11 ya mwaka huu.

Kikosi hicho kilichotangazwa na mwalimu Mayanga ni pamoja na magolikipa Aishi Manula, Peter Manyika na Ramadhan Kambwili.

Mabeki ni Gadiel Michael, Boniphace Maganga, Abdi Banda, Kelvin Yondani, Dickson Job, Erasto Nyoni na Nurdin Chona.

Wakati huo huo viungo waliochaguliwa ni pamoja na Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yasin, Raphael Daud, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Farid Mussa, Ibrahim Ajib, Mohammed Issa na Abdul Mohammed.

Aidha washambuliaji ni Mbaraka Yusuph, Yohana Mkomola, Mbwana Samatta na Elias Maguli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents