Michezo

Hawa ndio wachezaji kutoka katika klabu kubwa barani Ulaya wanaotaka kuzihama timu zao kwa hali yoyote ile, Pogba Lukaku ndani

Hawa ndio wachezaji kutoka katika klabu kubwa barani Ulaya wanaotaka kuzihama timu zao kwa hali yoyote ile

Dirisha la uchaguzi la majira ya joto barani Ulaya linaendelea kupamba moto na tayari kuna usajili wa mamilioni ya pauni unaohusisha wachezaji wenye majina makubwa umefanyika. Tayari miamba ya soka Uhispania klabu ya Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 120.

Atletico kwa upande wao wametumia kitita cha pauni milioni 126 kumsajili Joao Felix mwenye miaka 19 kutoka Benfica ya Ureno.

Lakini kama ilivyokuwa katika misimu iliyopita, kuna nyota wakubwa ambao wanataka kuhama ama wanahusishwa na uhamisho wa pesa nyingi lakini mpaka sasa bado hakuna kilichofikiwa.

Kuna nyota watatu, ambao wanaonekana kusaka uhamisho kwa nguvu zote. Nyota hao wamegoma kuungana ama wameachwa na tmu zao katika kipindi hichi cha kujiandaa na msimu mpya wa 2019/2020.

Laurent Koscielny

Koscienly

Huyu ni nahodha wa washika bunduki wa London klabu ya Arsenal.

Koscienly mwenye miaka 33 alijiunga na Arsenal mwaka 2010 na bado yungali na mkataba na klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu wa 2019/2020.

Hata hivyo ameweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.

Nahodha huyo ameenda mbali kwa kufikia hatua ya kugoma kusafiri na timu kwenye kwenye ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Arsenal imeeleza kusikitishwa kwake na hatua hiyo ikisema ni “kinyume kabisa na maelekezo yetu kwa mchezaji.”

Klabu tatu za nchini Ufaransa Bordeaux, Rennes na Lyon zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezji huyo.

Inaarifiwa kuwa Bordeaux imempa ofa ya mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji nyota wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amemtahadharisha Koscienly kuwa matendo yake ya sasa yatamfanya afute kumbukumbu zote nzuri alizojijengea kwenye mioyo ya mashabiki wa Arsenal kwa miaka 9.

Matthijs de Ligt

Matthijs de Ligt
Image captionMatthijs de Ligt

De Ligt naye ni nahodha na hajaungana na timu yake kwenye kambi ya maandalizi na anasaka uhamisho kwa nguvu kama Koscienly.

Tofauti baina yao ni kuwa, De Ligt ana baraka zote kutoka uongozi wa Ajax juu ya kile afanyacho.

Ajax kwa sasa wapo kwenye kambi ya maandalizi nchini Austria na nahodha wao amebaki Amsterdam akisubiri kukamilika kwa uhamisho kwenda moja ya klabu kubwa Ulaya.

Beki huyo wa kati kisiki ni kinda kiumri, ana miaka 19 tu, lakini ameiongoza Ajax kuchukua ubingwa wa Uholanzi msimu uliopita na kufika fainali ya klabu bingwa Ulaya ambapo walifubgwa na Liverpool.

De Ligt anawindwa na Barcelona, Juventus, Manchester United na Paris St-Germain.

Wiki iliyopita, rais wa klabu ya Barcelona Josep Bartomeu alisema anajua wapi mchezaji huyo atacheza msimu ujao.

Machampioni wa Italia klabu ya Juventus wanatajwa kuwa ndio wanaoweza kuinasa saini ya beki huyo na wanatarajiwa kutoa kitita cha pauni milioni 71.

Mauro Icardi

Icardi

Tofauti na De Ligt na Koscienly, Icardi alivuliwa unahodha wa klabu yake mwezi Februari mwaka huu.

Icardi naye hayupo kwenye kambi ya maandalizi ya Inter Milan na mshambuliaji huyo anatarajiwa kuuzwa kwenda klabu nyengine hivi karibuni.

Kama ilivyo kwa De Ligt Icardi amekubaliana na uongozi wa klabu hiyo kutokuwa sehemu ya kambi ya maandalizi.

Juventus ndiyo imekuwa ikitajwa zaidi katika mbio za kumsajili lakini mpaka saasa hakuna mazungumzo rasmi yaliyofanyika.

Napoli pia wanahusishwa na kumtaka sawia na AS Roma japo itakuwa vigumu kwa Icardi kwenda Roma ambao hawatashiriki Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Pogba na Lukaku

lUKAKU

Alipoulizwa na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya mustakabali wake katika kikosi cha Man United, Lukaku akajibu: “subirini wiki ijayo mtajua kitu.”

Lukaku amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu ya Inter Milan, na imefahamika kuwa uhamisho wake utategemea na kitakachotokea kwa Icardi.

Lukaku anapaswa kuondoka Man United

Hivyo endapo Icardi atauzwa wiki hii, ni dhahiri kuwa uhamisho wa Lukaku kujiunga na klabu hiyo utakuwa umeiva.

Lukaku ameambatana na kikosi cha United kwa sasa kilichopo kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchii Australia na Singapore.

Mshambuliaji huyo hakuwa na wakati mzuri msimu uliopita na amekuwa akishutumiwa kwa kushuka kiwango.

Pogba

Kwa upande wa Pogba kumekuwa na sarakasi za kutosha na zilikolea pala mchezaji huyo aliposema mwezi uliopita kuwa ”sasa inaweza kuwa muda mzuri wa kuhamia sehemu nyingine”.

Ni dhahiri kuwa si kocha Ole Gunnar Solskjaer wala uongozi wa Man United unaotaka mchezaji huyo nyota kuondoka Old Trafford katika dirisha hili la usajili la majira ya joto.

Wiki iliyopita, wakala wa mchezaji huyo Raiola aliliambia gazeti la The times kuwa mchezaji wake anataka kuondoka, na klabu hiyo inajua fika nia ya mteja wake.

Vilabu vya Real Madrid na Juventus vinaripotiwa kutaka kumsajili kiungo huyo Mfaransa mwenye miaka 26 japo hakuna kati yao ambaye amepeleka maombi rasmi ya kutaka kumnunua.

Chanzo BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents