Michezo

Hawa ndio waliotajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or

Messi akosekana kwenye orodha hii ya mwanzo

Tuzo za mchezaji bora wa dunia anatarajiwa kutangazwa mshindi mwaka huu katika Sherehe ambazo zinatarajiwa kufanyika mjini Paris nchi Ufaransa mnamo Desemba 3 2018. Nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, ni miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kushindania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.

Kuna pia wachezaji wa Chelsea Eden Hazard na N’Golo Kante ambao wameongezwa kuwania tuzo hiyo kubwa kabisa duniani. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale anayechezea Real Madrid pia ameorodheshwa kushindania tuzo ya Ballon d’or. Waandaji wa tuzo hiyo watakuwa wakiwatangaza wachezaji watakaowania tuzo hiyo mwaka huu kwa mafungu siku yoyote hadi wafike wachezaji 30.ambapo hadi hivi sasa wametajwa wachezaji 15 u.

Baadhi ya wachezaji Waliotangazwa kufikia sasa

  • Sergio Aguero (Manchester City)
  • Alisson (Liverpool)
  • Gareth Bale (Real Madrid)
  • Karim Benzema (Real Madrid)
  • Edinson Cavani (PSG)
  • Thibaut Courtois (Real Madrid)
  • Cristiano Ronaldo (Juventus)
  • Kevin de Bruyne (Manchester City)
  • Roberto Firmino (Liverpool)
  • Diego Godin (Atletico Madrid)
  • Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
  • Eden Hazard (Chelsea)
  • Isco (Real Madrid)
  • Harry Kane (Tottenham)
  • N’Golo Kante (Chelsea)

Kwa wachezahi wote hao 15 waliokishatajwa hadi hivi sasa klabu ya Real Madrid ndio inaongoza kwa kutoa wachezaji wengi ikiwa na wachezaji wanne hadi hivi sasa.

Ballon d’Or ni tuzo mashuhuri ambayo imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1956 na hutolewa kwa mchezaji bora zaidi wa mwaka wa kiume duniani.Mchezaji bora wa kike duniani pia atatunukiwa kwa mara ya kwanza.Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, aliyehamia Juventus kutoka Real Madrid majira ya joto. alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana.

Tuzo ya Ballon d’Or ambalo kwa Kifaransa maana yake ni Mpira wa Dhahabu imekuwa ikitolea na jarida la France Football ekila mwaka tangu 1956, na mshindi wa kwanza alikuwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England Sir Stanley Matthews.

Orodha ya wanaoshindania huandaliwa na wafanyakazi wa jarida hilo la Ufaransa, na mshindi kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na waandishi wa habari za michezo kutoka kote duniani. Kila taifa huwakilishwa na mwandishi mmoja. Kwa miaka sita, kulikuwa na ushirikiano na Shirikisho la Soka Duniani Fifa na jina lake likawa Fifa Ballon d’Or.

Hata hivyo, Fifa walifikisha kikomo ushirikiano huo mwezi Septemba 2016, na sasa kunatolewa tuzo ya Ballon d’Or na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa.Washindi wa tuzo za Fifa walitangazwa Septemba ambapo kiungo wa kati wa Croatia na Real Madrid Luka Modric alitawazwa mchezaji bora wa kiume duniani.

Mchezaji wa Brazil na Orlando Pride Marta alitawazwa mchezaji bora wa kike. Ronaldo alikuwa ameshinda tuzo hiyo mwaka 2016 na 2017.

Washindi wa awali wa Ballon d’Or: Ronaldo & Messi wametawala tangu 2008.

  • 2008Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Fernando Torres
  • 2009Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Xavi
  • 2010Lionel Messi, Andres Iniesta, Xavi
  • 2011Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Xavi
  • 2012Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Andres Iniesta
  • 2013Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Franck Ribery
  • 2014Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Manuel Neuer
  • 2015Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Neymar
  • 2016Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Antoine Griezmann
  • 2017Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents