Burudani

Hawa ndio wasanii 5 wa Hip Hop Bongo anaowakubali Rama Dee

Rama Dee amewataja wasanii watano wa muziki wa Hip Hop anaowakubali Bongo.

Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV kinachoendeshwa kupitia mtandao wa Facebook, muimbaji huyo amewataja rappers hao ni Joh Makini, Nick wa Pili, Bonta Maarifa, G Nako pamoja na Fid Q.

Hitmaker huyo wa Kipenda Roho, ameongeza kuwa anakubali sana kazi za msanii Damian Soul na kusema huyo ni msanii ambaye anajua muziki, pia anajua mpangilio mzuri wa muziki na kusema Damian ni mtu wa aina nyingine katika muzuki.

Amesisitiza pia kumkubali Barnaba Classic kwa kuwa ni msanii mzuri, huku akimtaja Ben Pol na Jux kua wasanii wazuri kwa sababu wanafanya kazi zao na watu wanazipenda na amewataka waendelee kufanya vizuri zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents