Uncategorized

Hawa ndiyo Watanzania 14 wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi wakiongozwa na Samatta

Timu nyingi za Taifa barani Afrika hunufaika zaidi kutokana na wachezaji wao wanaochezea sehemu mbali mbali nje ya nchi, hii inaaminika kuwa huleta changamoto mpya na uzoefu ndani ya vikosi vyao pindi wanapo liwakilisha taifa katika michuano.

This image has an empty alt attribute; its file name is NI-KWELI-600x401.jpg

Taifa kama Algeria limekuwa likinufaika zaidi na mfumo huo wa kuwa na wachezaji wengi wanaochezea kwenye klabu za nje ya nchi ambao wamekuwa na uzoefu mkubwa katika soka la ushindani, miongoni mwa mataifa mengine yanayonufaika ni Ghana, Cameroon, Misri na Nigeria.

This image has an empty alt attribute; its file name is stars.jpg

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa na Balozi wa Tanzania Kusini mwa Afrika Sylvester Ambokile na Kaimu Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Athuman Nyamlani wakiwa na wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na benchi la Ufundi

Wachezaji wa Tanzania siku za hivi karibuni wamekuwa wakipata soko kwenye nchi za nje huku idadi kubwa ikizidi kuongezeka.

Wachezaji wa Tanzania siku za hivi karibuni wamekuwa wakipata soko kwenye nchi za nje huku idadi kubwa ikizidi kuongezeka.

Miongoni mwa wachezaji wa Tanzania waliyopata nafasi ya kusajiliwa kwenye klabu za nje ya nchini ni pamoja na Mbwana Samatta.

Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania aliyepata nafasi ya kuzichezea klabu ya Simba, TP Mazembe ya DR Congo kisha kutimkia KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

This image has an empty alt attribute; its file name is samatta.jpg

Saimon Msuva mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Difaa El Jadida ambapo ametokea Dar es Salaam Young African.

This image has an empty alt attribute; its file name is MSUVAA.jpg



Abdi Banda ni beki kisiki wa timu ya Taifa ya Tanzania ambaye anaichezea klabu ya Baroka FC ya nchini Afrika Kusini akitokea Simba SC.

Thomas Ulimwengu mshambuliaji wa JS Saoura ya nchini Algeria raia wa Tanzania, akitokea Al- Hilal Club.

Image result for Thomas Ulimwengu JS SAOURA

Eliud Ambukile aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City amejiunga ambaye kwa sasa amejiunga na Black Leopards FC ya Afrika Kusini.

Rashid Mandawa mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya BDF XI  ya Botswana inayocheza ligi kuu ya nchi hiyo akitokea Mtibwa Sugar.

Hassan Kessy beki wa klabu ya Nkana FC ya nchini Zambia akitokea kwenye timu ya Yanga lakini pia akiwahi kuichezea Simba ya Tanzania.

Ally Hamisi Ng’anzi ni mchezaji wa klabu ya MFK VySkov ya daraja la pili barani Ulaya ambayo ipo Jamhuri ya Czech akitokea Singida United.

Adi Yussuph mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Solihull Moors Football Club ya nchini Uingereza akitokea Barrow  AFC ya hapo hapo England.

Himid Mao Mkami (Ninja) ni kiungo tegemezi wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Petrojet FC ya Misri akitokea Azam FC.  

Yahya Zayd mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anakipiga kwenye klabu ya Ismaily SC  ya nchini Misri akitokea Azam FC.

Shiza Ramadhan Kichuya winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya Simba ambaye kwa sasa ni mchezaji halali wa Enppi SC inayoshiriki ligi kuu nchini Masri.

Shaaban Idd Chilunda ni nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya CD Izarra inyoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania akitokea Azam FC.

Farid Mussa mshambuliaji mwenye kasi na uwezo wa kutembea na mpira kwenye winga ya kushoto na kulia na kuwafanya vibaya mno mabeki wazembe anakipiga kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania akitokea Azam FC.

Majina hayo 14 ya wanasoka wanaokipiga nchi mbali mbali duniani ni wale wanaozungumzwa tu midomoni mwa wapenda mpira lakini wapo wengi ambao hawafahamiki ila wanasukuma gozi huko huhaibuni na wengine wakiwa katika majaribio kama beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Job akiwa FC Arsenal Kyiv, Ndemla na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents