Tupo Nawe

Hawa wa Diamond atoa neno la shukrani kwa uongozi wa WCB (Video)

Msanii Hawa Said maarufu Hawa wa Diamond, amefunguka kwa mara ya kwanza kueleza hali ya afya yake ikiwa ni wiki chache toka asafirishwe na uongozi wa WCB kwenda nchini India kwaajili ya matibabu.

Mrembo huyo pia amemshukuru Mungu pamoja na Watanzania kwa dua zao kwani mpaka sasa anaendelea vizuri na uvimbe wa tumbo umeondoka kwa asilimia kubwa.

Mungu mkubwa hatimae Hawa anatabasamu tena. Acha Leo niamke usiku nisali kwa kumuombea @diamondplatnumz Mungu andelee kumfungulia na kumpunguzia mitihani ya kidunia hii iki ulichofanya hata nikuone umelala ndani ya chupa ya pombe siumii sana sababu naamini unahofu ya Mungu na unaupendo na watu. Basi kuna watu watanipigia wajue Hawa anarudi lini na sinto wajibu😂😂😂 ilaasante @shailaraveendran kwa moyo wako wa pekeee

Awali msanii huyo wa kike aliripotiwa kuumwa ugonjwa wa ini lakini alipofanyiwa vipimo nchini India walimkuta na ugonjwa wa moyo.

Uongozi wa WCB ambaye umesimamia matibabu wote ya mwanadada huyo hawajaeleza ni lini anarejea nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW