Haya ndio majina ya washiriki wa European Youth Film Competition 2017

Baada ya kuzinduliwa kwa shindano la kutengeneza filamu fupi lijulikanalo kama European Youth Film Competition 2017 na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya mapema mwezi Mei mwaka huu, hatimaye majina ya washiriki wapatao 35 yametangazwa.

Awali Afisa habari wa umoja huo Bi Susanne Mbise alipoongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa shindano hilo alisema watachagua washiriki 30 ambao watachuana katika kinyang’anyiro hiko.


Haya ndio majina ya washiriki waliotajwa kwenye shindano hilo

Washiriki hao wanatarajiwa kupewa elimu kwenye warsha itakayoandaliwa ili kuweza kujua juu ya utengenezaji wa filamu kwa kukutanishwa na mmoja wa waandaji wa makala ya “Tapis Rouge” aitwaye Kantarama Garighiri kutoka nchini Ufaransa, kabla ya kupata mshindi wa shindano hilo ambapo atatarajiwa kutangazwa mwezi Septemba katika maonesho ya filamu.

Shindano hilo linawajumuisha vijana wa Kitanzania wenye umri kuanzia miaka 18-35 na jumla ya shilingi milioni 15 za kitanzania zitatolewa kwa washindi wa shindano hilo, mshindi wa kwanza atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 7 na wa pili milioni 5 na mshindi wa tatu milioni 3.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW