Michezo

Haya ndio makombe 20 aliyobeba Roger Federer kwenye tenisi tangu mwaka 1998

Hakuna furaha kubwa kama kufanikiwa katika malengo yako. Roger Federer kwa sasa kicheko chake mpaka jino la mwisho linaonekana baada ya jana (Jumapili) kufanikiwa kushinda taji lake la sita katika michuano ya Australian Open na la 20 katika mashindano yote makubwa aliyowahi kushiriki tangu mwaka 1998 alipoanza kushiriki mashindano ya mchezo wa tenisi.

Ukiachana na mataji ya Australian Open, taji ambalo ameshinda mara nyingi zaidi bingwa huyo ambaye nashika namba moja kwa ubora katika viwango vya mchezo huo duniani, ni lile la Wimbledon ambalo ameshinda mara nane na matano ya US Open.

Haya ndio mataji 20 ambayo Roger Federer ameshinda mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 36.

Wimbledon 2003

Roger Federer alianza kushinda taji lake la kwanza mwaka 2003 ambalo lilikuwa ni la Wimbledon ambapo alimfunga Mark Philippoussis kutoka nchini Australia kwa seti 7–6(7–5), 6–2, 7–6(7–3).

Australian Open 2004
Mwaka 2004 Federer alishinda taji lake la pili ambapo ilikuwa katika mashindano ya Australian Open kwa kumfunga Marat Safin wa Urusi kwa seti 7–6(7–3), 6–4, 6–2. Wakati Roger ananyakuwa kombe hilo hiyo ilikua ni mara yake ya saba kushiriki michuano hiyo mikubwa ya mchezo wa tenisi mbapo mra sita zote alizowahi kushiriki hakufanya vizuri.

Wimbledon 2004
Maka 2004 ulikuwa mzuri kwa mchezaji huyo ambapo baada ya kushinda taji la Australian Open alifanikiwa tena kushinda taji la Wimbledonkwa kumfunga Mmarekani ambaye alikuwa katika kiwango bora kwa wakati huo, Andy Roddick kwa seti 4–6, 7–5, 7–6(7–3), 6–4.

US Open 2004

Kuonyesha kuwa mwaka 2004 ulikuwa wa neema kwa Rogger Federer, mchezaji huyo alifanikiwa kunyamakuwa mataji matatu. Hilo la tatu lilikuwa ni US Open ambpo pia lilikuwa ni taji lake la nne tangu aanze kucheza mchezo huo. Federer alifanikiwa kumfunga Lleyton Hewitt wa Australia katika fainali hiyo kwa jumla ya seti 6–0, 7–6(7–3), 6–0.

Wimbledon 2005
Roger Federer alifanikiwa kunyakuwa taji lake la pili la michuano ya Wimbledon mwaka 2005 ambapo pia lilikuwa ni taji lake la tano kwa kumfunga Andy Roddick wa Marekani kwa seti 6–2, 7–6(7–2), 6–4. Lakini kubwa zaidi ilikuwa ni fainali ya pili ya michuano hiyo kwa Federer kumfunga Roddick katika hatua ya fainali.

US Open 2005
Mwaka huo huo wa 2005 Roger alinyakuwa taji jingine la US Open kwa kumfunga Andre Agassi kwa jumla ya seti 6–3, 2–6, 7–6(7–1), 6–1. Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa mchezaji huyo kunyakuwa taji hilo la US Open.

Australian Open 2006
Makali ya Roger Federer yaliendelea kutesa mwaka wa 2006ambapo alinyakuwa taji la Australian Open kwa mara ya pili kwa kumfunga Marcos Baghdatis wa Cyprus katika fainali kwa seti 5–7, 7–5, 6–0, 6–2.

Wimbledon 2006

Federer alikutana na Rafael Nadal katika fainali ya pili mwaka 2006. Mwaka huo huo Nadal alifanikiwa kumfunga Roger katika fainali ya michuano ya French Open. Hata hivyo mwaka huo huo Federer alilipiza kisasi katika fainali ya michuano ya Wimbledon kwa kumfunga Nadal kwa seti 6–0, 7–6(7–5), 6–7(2–7), 6–3 na kunyakuwa taji hilo kwa mara ya nne.

US Open 2006
Mwaka 2006 Roger Federer aliendelea kukimbiza kwa kunyakuwa taji lake la tatu la US Open na likiwa ni taji lake la tatu katika mwkaa huo na la tisa tangu aanze kucheza mchezo wa tenisi. Wakati Roger ananyakuwa taji lake hilo la US Open alifanikiwa kumfunga Andy Roddick kwa seti 6–2, 4–6, 7–5, 6–1.

Australian Open 2007
Roger Federer alianza mwaka 2007 kwa kicheko baada ya kumfunga Fernando González kutoka Chile kwa seti 7–6(7–2), 6–4, 6–4 na kunyakuwa taji la Australian Open.

Wimbledon 2007
Rafael Nadal alimfunga Roger Federer kwenye hatua ya fainali ya michuano ya French Open mwaka 2007 kwa seti 3–6, 6–4, 3–6, 4–6. Mwaka huo huo walikutana tena katika fainali ya michuano ya Wimbledon ambapo Federer alilipiza kisasi kwa kushinda kwa seti 7–6(9–7), 4–6, 7–6(7–3), 2–6, 6–2.

US Open 2007
Hasira za Federer kwa mwaka huo wa 2007 ziliendelea mpaka kwenye michuano ya kombe la US Open ambapo alimchakaza Novak Djokovic katika hatua ya fainali kwa jumla ya seti 7–6(7–4), 7–6(7–2), 6–4. Hilo lilikuwa ni taji la nne la michuano hiyo kwa Roger Federer kushinda.

US Open 2008

Mwaka 2008 ulikuwa mbaya sana kwa Federer kwa kutolewa katika fainali mbili ikiwemo French Open na Wimbledon, na pia alitolewa katika hatua ya nusu fainali ya Australian Open. Hata hivyo mchezaji huyo alifanikiwa kuambulia taji moja pekee la US Open kwa kumfunga Andy Murray katika hatua ya fainali kwa seti 6–2, 7–5, 6–2.

French Open 2009
Federer alirudi tena mwaka 2009 kwa kunyakuwa taji la French Open ambalo alilipoteza mwaka 2008 kwa kufungwa katika hatua ya fainali na Rafael Nadal. Roger alimfunga Robin Söderling wa Sweden kwa seti 6–1, 7–6(7–1), 6–4 na kufanikiwa kubeba taji hilo la michuano ya French Open.

Wimbledon 2009
Andy Roddick ni miongoni mwa wacheza tenisi ambao wamekutana mara nyingi na Roger Federer katika hatua ya fainali. Mwaka 2009 Roddick alijikuta akipoteza fainali yake ya nne mbele ya Federer katika michuano ya Wimbledon kwa seti 5–7, 7–6(8–6), 7–6(7–5), 3–6, 16–14.

Australian Open 2010
Roger Federer alirudi kufanya vibaya mwaka 2010 kwa kushinda kwa kushinda taji moja ambalo lilikuwa la Australian Open. Federer alifanikiwa kumfunga Andy Murray kwa seti 6–3, 6–4, 7–6(13–11) na kushinda taji hilo ambalo lilikuwa la tano.

Wimbledon 2012
Andy Murray hajawahi kumfunga Roger Federer katika fainali yoyote ya mchezo wa tenisi ambayo wamewahi kukutana. Mwaka 2012 wachezaji hao walikutana tena kwa mara ya tatu na Federer aliibuka mshindi kwa seti 4–6, 7–5, 6–3, 6–4 na kufanikiwa kushinda taji la michuano ya Wimbledon 2012.

Australian Open 2017
Roger Federer na Rafael Nadal wamekutana mara tisa katika fainali tofauti tofauti za michuano ya tenisi. Nadal ameshinda katika fainali sita huku Federer akishinda fainali tatu ikiwemo ya Australian Open mwaka 2017 ambapo alishinda kwa seti 6–4, 3–6, 6–1, 3–6, 6–3 na kutwaa kombe la michuano hiyo.

Wimbledon 2017
Marin Čilić kutoka Croatia anaweza akawa ndio mpinzani mpya wa Roger Federer kwa kipindi hichi. Kwa mara ya kwanza wawili wao walikutana katika fainali ya michuano ya Wimbledon mwaka 2017 ambapo Federer aliweza kuibuka mshindi wa kombe hilo kwa jumla ya seti 6–3, 6–1, 6–4.

Australian Open 2018

Baada ya kufungwa kwenye fainali ya Wembledon mwaka uliopita, Marin Čilić amechakazwa tena mwaka huu na Roger Federer katika fainali ya Australian Open ambayo imemalizika siku ya Jumapili ya January 28. Katika fainali hiyo Federer alishinda kwa seti 6–2, 6–7(5–7), 6–3, 3–6, 6–1 na kukamilisha idadi ya vikombe 20 ambavyo amewahi kushinda katika michuano yote ya tenesi tangu alipoanza kushiriki mwaka 1998.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents