Habari

Haya ndio mambo manne yanayotishia usalama kwa nchi za Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema kuna aina nne za mambo yanayotishia usalama katika nchi za Afrika Mashariki.

Balozi Augustine Mahiga

Akitaja mambo hayo, Balozi Mahiga amesema ni ugaidi, uharamia, na majanga mengine kama matetemeko ya ardhi na masuala ya kisiasa.

Balozi Mahiga amesema hayo juzi (Ijumaa) wakati akifunga mafunzo ya ‘Ushirikiano Imara 2017’, jijini Dar es Salaam, ambayo nchi za Afrika Mashariki zimeshiriki ikiwemo na Tanzania.

Amesema licha ya mambo hayo kuwa tishio, bado majeshi ya usalama yapo imara, na Tanzania mpaka sasa haijafikia hatua ambayo inatishia amani.

Akizungumzia mafunzo hayo, Balozi Mahiga amesema mafunzo hayo yanaleng la kudumisha uzalendo na kubadilishana mawazo na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Zoezi hili ni la muhimu sana na sehemu ya itifaki. Mwaka jana yalifanyika nchini Kenya. Leo ni fursa ya uongozi wa juu kabisa katika majeshi ya Afrika Mashariki kukaa pamoja na kufanya mazoezi pamoja na Tanzania tumekuwa wenyeji.” amesema Balozi Mahiga.

Naye Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi na weledi katika majeshi.

Chanzo:HabariLEO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents