Michezo

Haya ndio maneno ya Bekham kwa Zlatan baada ya rekodi yake ya kufunga magoli 500

Haya ndio maneno ya Bekham kwa Zlatan baada ya rekodi yake ya kufunga magoli 500

Mchezaji wa zamani wa Manchester United,Real Madrid,Psg na timu ya taifa ya England David Beckham amemsifia Mchezaji wa LA Gallaxy Zlatan Ibrahimovic kwa kufikisha goli 500 katika karia yake ya uchezaji wa mpira.

Zlatan alifunga goli la 500 kwa staili ya aina yake siku ya jumamosi wakati timu yake ya LA Gallaxy ikicheza na Toronto Fc ingawa timu yake ilifungwa kwa jumla ya goli 5-3 huku Zlatan akifunga goli lake dakika ya 43.

Beckham na Zlatan walishawahi kuchezea timu moja msimu 2013 hapo ndipo urafiki wao wa karibu ulipoanzia,marafiki hawa wawili waliweza kuleta gumzo kwenye mitandao ya kijamii siku ambapo England alikutana na Sweden katika michuano ya kombe la dunia lililofanyika Urusi mwezi julai,walipotambiana kuwa kila mmoja atamtoa mwenzake out na kumnunulia chakula popote anapotaka indapo timu yake itashinda.

Beckham amempongeza sana Zlatan kupitia video aliyoipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na uzungumza maneno mengi sana kwa kusema kuwa “anajivunia mno kuwa na rafiki kama Zlatan pia kucheza timu moja”

Haya ndio maneno ya Beckham kwa Zlatan:-

Zlatan amefanikiwa kufunga magoli mengi zaidi katika klabu ya PSG akifunga jumla ya goli 122,Intamilan 88,Ajax 74,Juventus 70,Manchester United 33,AC M ilan 32,Malmo 40, Barcelona 29,Gallaxy 22 na wakati yuko kwa mkopo AC Milan 29,lakini pia timu ya taifa alifanikiwa kuifungia jmla ya magoli 166 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa taifa la Sweden.

By Ally Juma

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents