Burudani

Haya ndio maneno ya Ronaldo baada ya kutambulishwa Juventus

Haya ndio maneno ya Ronaldo baada ya kutambulishwa Juventus

Mchezaji mpya wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana ameweza kutambulishwa rasmi katika klabu hiyo na kuchukuliwa vipimo vya kiafya.

Baadhi ya kauli alizozitoa mshambuliaji huyo wakati anazungumza na waandishi wa habari zimetafsiriwa tofauti na wadau mbalimbali wa michezo.

“Mimi ni tofauti na wachezaji wengine wote ambao wanafikiri kazi yao iko juu ya umri wangu,” alisema Ronaldo.

Aliongeza, “Ninataka kuonyesha kwamba mimi si kama wengine, mimi ni tofauti, ni wakati mzuri sana kwangu na klabu kwa sababu mimi sina miaka 23, bali nina miaka 33. Umri wangu sio tatizo sana najisikia vizuri sana,najisikia kuhamasika, na nina furaha,”

Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kwa kitita cha  Euro mil 100 amesema atajumuika kwenye mazoezi na wachezaji wenzake wa timu hiyo Julai 30 mwaka huu.

Ronaldo amefanikiwa kufunga magoli 450 katika klabu ya Real Madrid kwa muda wa misimu 9 huku akiisaidia kutwaa mataji 15 mataji manne ya UEFA na mawili ya Laliga,huku akichukua tuzo ya mchezaji bora Duniani Ballon d or mara tano.

by Ally jei.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents