Habari

Haya ndio maoni ya mashabiki wa Crazy GK baada ya kuandikiwa barua ya wazi ‘Tunamtaka yule wa enzi za ‘Sista Sista’ na ‘Hii Leo’

Jumatano ya wiki hii ni siku ambayo nadhani hata wale ambao huwa hawasikilizi sana radio mchana kutokana na kubanwa na majukumu lakini ni wapenzi wa muziki wa zamani na wapenzi wa rapper mkongwe Gwamaka aka Crazy GK, huenda hata walijipa mapumziko ya masaa mawili kwaajili ya kusubiri kuusikia wimbo mpya wa mkali huyo wa ‘Hii Leo’ na member wa kundi la East Coast Team.

GK1

Siku moja baada ya wimbo huo mpya unaoitwa’Baraka au Laana’ kutambulishwa kupitia XXL ya Clouds FM na vituo vingine vya radio kuna shabiki wa damu aitwaye SKY alitoa hisia zake za dhati na kuamua kumuandikia barua GK iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Tunamtaka yule wa enzi za ‘Sista Sista’ na ‘Hii Leo’.

Zifuatazo ni comments za mashabiki wengine wa Gwamaka aka GK kuhusu barua hiyo iliyozungumzia ujio mpya wa mwana mpotevu huyo GK.

Wynjones Kinye: Wynjones Kinye – Works at SAUT

KIROHO SAFI
its either hushauriki au hukuwapa nafasi watu walio wazi wakushauri…SIJUI KIPI NI SAHIHI.

Ulipotea ukiwa KILELENI…kurudi kileleni unahitaji watu wa kukuambia ukweli, sio kukushabikia KINAFKI au kukushabikia kwasababu wako excited sana na ujio wako au heshima yao kwako.

Nashawashika kuamini kuwa wapo ambao walikusindikiza huku hawajui hata ni nini kinaenda kusikika, kwa waliofuatilia ile interview watakuwa wanakumbuka alichoongea FA baada ya wewe kuuelezea wimbo (baada ya wimbo kusikika)…

Sidhani kama siku ile ilikuwa nzuri kuanza mambo ya ECT vs TMK…ni kweli ulimwagiwa mafuta nawe ukaanza kulipuka, ulilipuka vibaya ukiwa hujui kuwa tayari asilimia kubwa ya fans wako walikuwa disappointed na kile ulichowaletea.

Mimi ni nani unisikilize? Sisemi unisikilize, nataka unielewe kuwa unahitaji watu wa kukuambia ukweli kama alivyofanya sky….UKWELI ulio wazi ni kwamba U CANNOT SING, U REALLY CAN’T.

Rudi chimbo au pekua stock yako ulete track nyingine, sio ya kuimba lakini.


Rogers Mwikwabe • Works at DStv

Nilidhani mie mwenyewe ndo nmeona dis, Na support 4 sure tunamtaka yule GK wa enzi zile, ukikomaa na ile ile style yako utakimbiza tu..

Montana Capaccino Grand Stunner -Singer-songwriter at TAYLOR GANG, PAPER PLANES!
#KIUKWELI KABISA NILIKUWA NA HAMU YA KUMSIKIA GK LAKINI SI GK HUYU MI NAMTAKA BOKASA, GK SAUTI YA MANKA, GK SIMBA WA AFRIKA, GK KIRAKA, GK YULE HII NGOMA KALI SANA UNGEPITA KATIKA MITINDO YAKO ILE NAAMIN MAWAZO HAYA YATAKUFIKIA.
FANYA MABADILIKO HARAKA IWEZEKANAVYO KWA MTINDO HUU NATURE HUMUWEZII.

Rick John Sanga
Naunga mkono hoja si ktk uvivu wa kufikiria la hasha ila jamaa umeelezea ambacho ning’eelezea pia
Rashidi Mugisha
That’s true dude said coz naona sie GK ambao watu wamemzoea kumskia mbona kama kakulupuka kwenye hiyo nyimbo kama ana rudi kujifunza mziki.

Ally Hussain – COTC KILOSA
Bado hujakata kiu ambayo nlonayo tangu ulipoondoka na album yako ya mwisho.

Osiana Bryson Mwakyambo- Managing Partner at OSS.
KIUKWELI KAMA USHABIKI BASI MI JAMAA CKU ZOTE AMEKUA NI MC WANGU NAMBA MOJA NA NIMEFURAHISHWA SANA NA UJIO WAKE NIMEISIKILIZA NGOMA ZAIDI YA MARA SITA AISEE KAKA KAKAZA SANA HONGERA BRO NA NAKIRI SINTAUNGA MKONO MAANDAMANO YA MWANDISHI WA BARUA NAONA KWENYE KUMI TISA WANASEMA WIMBO MZURI SANA SASA SIJUI HIYO BARUA ILA SISHANGAI KILA MTU ANAMAONI YAKE.

Moses Mayrick Mwakalobo • The University Of Dodoma

wimbo ni mzuri ndio lakini kwenye Rap G.K ana uwezo mkubwa kushinda huu wimbo aliotoa,

Agness Slashday Michaely Jerome -Presenter at Safari Radio 89.9 Fm

me naona anazingua tu kama vp akatafute kazi ya kufanya aachane na mziki kabisa koz haeleweki.
Sophia Abbasi • Dar es Salaam, Tanzania
Wapi sauti ya manka huwa naisikia? Gk we mkaliiiii, rudi kama zamani uwakimbize

Iddy MJ • Udom
True,tunamtaka GK yule tuliemzoea…

Joshua Myinga • Mposec
Badiriik ngoma yko mpya cjapokea kwa mikono 2.

kama hukupata nafasi ya kuisoma barua kwa wazi kwa Crazy GK ingia HAPA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents