Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Haya ndio maoni ya Watanzania kuhusu mabadiliko ya ada wanazotozwa wasanii na BASATA

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu BASATA watangaze mabadiliko ya tozo za ada za usajili kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva kumeibuka na maoni tofauti tofauti wengi wao ambapo wadau na wasanii wameonekana kupokea mabadiliko hayo kwa mtazamo hasi.

Gumzo kubwa kwa wasanii sio gharama za usajili kwani gharama hizo zimeonekana kushuka kutoka tsh 75,000/= hadi 20,000, bali gumzo ni kwenye gharama za makato kwenye tangazo atakalofanya msanii husika na gharama za matamasha.

SOMA ZAIDI-BASATA watangaza mabadiliko ya bei za usajili, MaDJ na Wasanii wapumua, Makampuni bei juu

Kwa mujibu wa mabadiliko mapya kutoka BASATA kampuni itakayomtumia msanii itatakiwa kulipa tsh milioni 5 kwa kila tangazo itakalofanya na msanii husika.

Kufuatia mabadiliko hayo Bongo5 imekusanya maoni ya Watanzania wa kawaida na wadau wa muziki kupitia kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wao wameonekana kushangazwa na tozo hizo hasa ya milioni 5 huku wengine wakiwashauri BASATA kukaa upya na Wasanii na wadau wengine wameenda mbali na kuingiza suala hilo na mambo ya kisiasa.

ndamao Ni lazima mlipe Kodi wasanii, Haiwezekani mnatakata wakati Watanzania tunazidi kupauka na kuwa hohehahe….lazima wote tuisome namba.

chuwagift Mtanyoooka tu na muda ukifka nendeni mkaimbe tena mbele kwa mbele!! Kanyaga twende mjomba

daxiyeerico@basata.tanzania kwani basata ndo wanafanya tangazo au anafanya msanii kwani basata ndiyo management ya msanii siku hizi??

nyau_19 Suala la kutaka kampuni zilipe basata 5mil kwa kila tangazo ambalo watamtumia msanii ni kutaka kuzidi kuminya mianya kwa wasanii wetu kupata fursa ya matanzano……mimi nilidhani sababu wasanii wanalipa kodi basi kufanya matangazo na ayo makampuni ndio kutumika kwa kodi zao uko maana show zenyewe asaivi ndio kama tunavyo ona media hii haipatani na uyu basi uyu hana show kwenye media ile, tunawaua wasanii wetu. #IloveTanzania

nellyblive BASATA HAMJANIJIBU….. HIVI MNATAKA KUUWA WASANII….MNATAKA WAFE NA NJAA Haya Iyo Ilkuwa Njia Nyingine Ya Wasanii Kujipatia Kipato….. Big Up @nchakalih Kasaidia Wasanii Wote…. Wa Hip Hop Na Bongo Fleva Kuwa Na Usawa Kwenye Matangazo….. Mnataka Hizi Kazi Tukazifanyie Njee….. MLIKAA NA WADAU GANI HAMJANIJIBU.

chattslatest Hivi hapo mnalinda na kutetea maslahi ya wasanii au mmelenga kujinufaisha wenyewe kupitia juhudi za wasanii!!? Hamuoni Kama hayo makampuni yataanza kukwepa kuwatumia wasanii kwenye matangazo yao na wasanii mnaosema mnawatetea wakakosa fursa?

nicodemgram Mnatoza million 5 hivi mnajua matangazo yenyw wanapewa bei gani, hii cyo haki kabsa

chattslatest Hivi hapo mnalinda na kutetea maslahi ya wasanii au mmelenga kujinufaisha wenyewe kupitia juhudi za wasanii!!? Hamuoni Kama hayo makampuni yataanza kukwepa kuwatumia wasanii kwenye matangazo yao na wasanii mnaosema mnawatetea wakakosa fursa?

Hata hivyo, baadhi ya wasanii wa muziki na waigizaji akiwemo Steve Nyerere, Wakazi na Nikki wa Pili tayari wamepinga tozo hiyo kwa kile walichoeleza kuwa tozo hiyo itaanza kupoteza dili za wasanii kufanya kazi na makampuni.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW