Bongo5 ExclusivesPicha

Hayati Brenda Fassie leo kuperform live kwa hologram iliyogharimu tshs bilioni 1.7

Hayati Brenda Fassie leo anatarajia kuletwa hai kwenye stage nchini Afrika Kusini kwa njia ya hologram. Brenda aliyefariki mwaka 2004 ataungana na mwanae Bongani kutumbuiza kwenye ‘Hansa Pilsner Festival of Legends’ huko Newtown, Jo’burg.

3914781873_8d1cc6b2a7

Technolojia hiyo ya hologram itatumika kwa mara ya kwanza nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti za mtandaoni, watalaam wa mambo ya sauti na picha zimewachukua wiki sita kutengeneza hologram ya Brenda na kugharimu Rand milioni moja sana na zaidi ya shilingi bilioni 1.7 za Tanzania.

Mwaka jana Tupac aliperform kwenye show ya Coachella nchini Marekani kwa kushirikiana na Snoop Dogg na Dr Dre. Pia mwaka 2008, Will I Am aliweka historia kwa kuhojiwa kwa mara ya kwanza kupitia hologram na CNN.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents