Soka saa 24!

Hazard akinzana na Maurizio Sarri kwa hili, akiri hata Mourinho na Antonio Conte walimtaka kufanya kama hivyo, asisitiza yeye sio mbinafsi

Meneja wa klabu ya Chelsea, Maurizio Sarri amemtaka mshambuliaji wake, Eden Hazard kufunga magoli mengi zaidi kadri awezavyo lakini inaonekana anachofanya ni tofauti na alichoshauriwa kufanya.

Hazard mpaka sasa amefunga jumla ya magoli 12 premier league msimu huu ikiwa ni tofauti na kipindi cha mwaka 2016/17 ambapo aliweka wavuni mabao 16.  

Mbali na idadi hiyo ya magoli 12 aliyofunga mpaka sasa, Hazard pia ametoa pasi 10 za mwisho zilizochangia kupatikana kwa mabao ‘assists’ kwenye mechi 24 za ligi alizocheza na kuuwambia mtandao wa The Times kuwa yeye si mbinafsi.

”Hivi ndivyo uzaifu wangu wa mimi kutokuwa mchezaji bora duniani. Kocha kama Jose Mourinho, Antonio Conte na sasa Sarri wakihitaji nifunge mabao 40 hadi 50 kwa msimu lakini naweza kufanya hivyo ?, sina hakika.”

Eden Hazard ameongeza ”Pengine wanafikiri naweza lakini mimi mwenyewe binafsi nafahamu siwezi, ila nitajaribu.”

”Nahitaji kweli kuwa staa, lakini ningependa pia nitoe pasi na wenzagu wafunge, na hii siyo mimi bali ni kwakila mmoja kwa sababu lengo langu ni kuisaidia timu kushinda.”

Hazard mpaka sasa ameshinda jumla ya mataji mawili ya Premier League ndani ya miaka yake sita na nusu tangu kuwepo kwake Stamford Bridge, lakini pia akishinda mataji ya League Cup, FA Cup na Europa League.

Wengi wanaamini huwenda huu ukawa msimu wake wa mwisho kwa nahodha huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28, Hazard ndani ya jiji la London na kutimkia Real Madrid kama tetesi za usajili zinasema. 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW