Michezo

Hazard na Real Madrid mambo safi, Mateo Kovacic ahusishwa kurahisisha mambo Stamford Bridge

Klabu ya Chelsea huwenda ikampoteza nyota wake Eden Hazard wakati wa usajili wa majira ya joto baada ya mchezaji huyo kufikia baadhi ya makubaliano na Real Madrid.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kutimkia Hispania.

Mkataba wa Hazard na Blues unatarajia kufikia tamati mwaka 2020, na kwa sasa klabu hiyo ya London ipotayari kumuachia kufuatia dili lake na Madrid.

Hata hivyo nyota huyo hana muda mrefu wa kuitumikia Premier League kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania anatarajiwa kuondoka usajili huu unaokuja wa majira ya joto.

Kwa mujibu wa kituo cha radio cha Onda Madrid, Real wamefikia makubaliano na Hazard na kwa sasa anafanya taratibu za kukamilisha swala hilo ili kutua Bernabeu.

Onda Madrid imesema kuwa upande wa The Blues umehitaji kiasi cha uro milioni 170 kwaajili ya kukamilisha usajili huo huku Madrid ikikataa kwa madai haiwezi kulipa kiasi hicho cha fedha kwa mchezaji ambaye anaingia mwaka wake wa mwisho wa kumaliza mkataba.

Miamba hiyo ya LaLiga imeripotiwa kuwa bado inamatumaini ya kumnasa Hazard kupitia  kubadilishana kwa kiungo wake, Mateo Kovacic ambaye yupo Stamford Bridge kwa mkopo.

Hata hivyo meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri amewahi kuripotiwa wiki hii akisema kuwa klabu hiyo ipotayari kuingia mkataba na Hazard huku akisema kuwa wanachosubiri ni maamuzi yake kama atahitaji kuendelea kuwepo ama kuondoka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents