Bongo Movie

Hemedy PHD adai ataachia video sita (6) za muziki kabla mwaka haujaisha

Msanii wa muziki na filamu ,Hemedy Suleiman amefunguka kwa kudai kuwa ndani ya mwaka huu atatoa video sita (6) ili kutoa burudani zaidi kwa mashabiki wake.

hemed-8

Akizungumza jana na The Cruise ya East Africa Radio, Hemedy , amedai kuwa kuanzia mwezi huu wa 6 mpaka wa 12 atakuwa anatoa video kila mwezi.

“Mwaka huu nina plan kwamba mpaka mwaka unaisha nimeachia video zangu sita (6) ,kuanzia huu mwezi wa sita(6) mpaka wa kumi na mbili(12) , kwa maana nina mazoea ya kila mwezi kupresent video mpya, yaani hayo ni malengo ambayo nimeyaweka, nataka tu ile attention kwamba ‘this guy right now is busy na yupo serious na muziki industry’, Kwaiyo kinacho happen sasa hivi, nipo kwenye shooting ya video yangu ya tatu, ngoma ambayo imerekodiwa Say Record, tunaishoot mimi na jamaa wa Kwetu studio kwa sababu jamaa hao ndio nimeamua kuwapa kazi hiyo. Pia nipo kwenye mchakato wa kushoot tano nyingine. Acha hii ambayo inatoka week hii, kwahiyo watu wategemee kila mwezi watapata video mpya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents