Bongo Movie

Hemedy PHD kufanya collabo na Ray C

hemed

Habari ya kuimarika kwa afya ya Ray C aliyemtembelea rais Jakaya Kikwete katika ikulu ya Dar es Salaam wiki hii kumshukuru kwa kugharamia matibabu yake, iliwafurahisha mashabiki wake wengi, lakini zaidi ni Hemedy PHD.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, msanii huyo wa R&B ambaye pia ni muigizaji wa filamu, amefanya ama anatarajia kufanya ngoma na Ray C ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila.

“Dar thanx god Ray C amerecovery tumsubirie kwenye ngoma yangu mpya very soooon inaitwa I miss you very hoot track production inafanyijka Kiri Rec na Cnine,booooooonge la hit,” aliandika Hemedy.

Hivi sasa Hemedy ana wimbo mpya mwingine uitwao Going Crazy uliorekodiwa kwenye studio za B’Hits.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents