Michezo

Henry Joseph arudi Norway Majeruhi


Kiungo wa Taifa Stars Henry Joseph Shindika ameondoka nchini na kurejea Norway katika timu yake ya Konggsvinger na kuahidi kupambana kwa kila hali ili timu hiyo isishuke daraja.

Henry alionyesha kiwango kizuri katika mechi ya Stars dhidi ya Algeria ijumaa iliyopita akajikuta akitolewa uwanjani kwa maumivu ya misuli ya vigimbi hivyo kushindwa kuendelea na mchezo dakika ya mwisho na nafasi yake kuchukuliwa na Erasto Nyoni.

Bado maumivu ni makali lakini nikifika Norway nitatibiwa vizuri na nitaweza kucheza mechi ya Jumapili naweza nikacheza ila nitaangalia afya yangu itakavyo kuwa alisema kiungo huyo wa zamani wa Simba.

Narudi Norway sasa na nitaelekeza nguvu kuisaidia timu yangu isishuke daraja maana hali ni mbaya mpira tunacheza lakini tatizo kubwa tunalo tunaruhusu magoli ya kusawazisha.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents