Habari

Henry Mdimu ateuliwa kuwa msemaji wa Kili Music Awards Academy

Leo tarehe 28 Aprili 2012, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager amemtambulisha kwa waandishi wa habari, Mhariri wa habari za burudani wa gazeti la mwananchi, na mmiliki wa Blog ya Mdimuz, Bw Henry Mdimu kuwa msemaji mkuu wa Academy ya Kili Music Awards kwa msimu huu wa mwaka 2013/14 katika ukumbi wa safari Pub uliopo ilala, katika bohari ya kampuni ya bia Tanzania, TBL

IMG_1311

Mdimu ambaye amekuwa Mjumbe wa Academy kwa mwaka wa nne sasa, pia mwaka jana aliongoza jopo la majaji katika kutafuta vipaji vipya vya muziki wa kizazi kipya, katika ziara iliyoitwa Kili Talent Search Tour ambapo wasanii kama Young Killer na Neylee walipatikana kupitia msako huo ulioendeshwa katika mikoa mitano.

Uteuzi wa mdimu umepokelewa kwa mtazamo chanya na wadau huku kila mmoja akiamini uchapakazi wake na uadilifu alionao katika medani ya sanaa ndio uliopelekea mpaka Baraza la sanaa la taifa, ambao ndio wamiliki halali wa tunzo hizo, kulitaja jina la mdau huyu ambaye mwaka huu ametimiza miaka 17 tangu kuanza kazi ya uandishi wa habari za burudani.

Mdimu ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Times FM, baada ya uteuzi huo alionekana akiwa mtu mwenye kuangalia uwezekano wa kuirasimisha fani ya muziki kuwa ajira rasmi yenye kuheshimika.

“Hili ni daraja nimepandishwa, lakini nataka kuwaambia ndugu zangu kwamba nitaitumia hii nafasi kama jukwaa la kusemea wasanii wetu wa Tanzania, ili wafikie hadhi zao ambazo mpaka sasa, wengi wao hawajazitambua”.

Mdimu ambaye ni mjukuu wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Watangatanga, Mzee Herry Mdimu ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja na mwakani atachaguliwa msemaji mwingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents