Michezo

Henry, Neville na Carragher watabiri bingwa wa msimu mpya wa EPL

Wachezaji wa zamani wa vilabu vya ligi kuu ya Uingereza na wachambuzi wa kituo cha Sky Sports akiwemo Thierry Henry, Gary Neville na Jamie Carragher wametabiri bingwa wa kombe hilo kwa msimu ujao wa ligi utakaoanza Agosti 13 mwaka huu.

Caragher

Msimu uliopita vilabu vyote vikubwa vilivyotegemewa kufanya vizuri kwenye ligi hiyo vilidondokea pua kwa kushindwa kunyakuwa kombe hilo huku timu ya Leicester City iliyoshindwa kupewa nafasi mwanzoni mwa ligi hiyo ya msimu uliopita ikifanikiwa kunyakuwa kombe hilo.

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry ameipa nafasi timu ya Manchester City kushinda kombe hilo kwa msimu ujao lakini bado anamatumaini na timu yake ya Arsenal kufanya vizuri kutokana ilifanikiwa kushika nafasi ya pili msimu uliopita ikivunja mwiko wa muda mrefu uliozoeleka kwa timu hiyo kushika nafasi ya nne.

Aidha mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher ameipa nafasi timu ya Manchester City kufanya vizuri kwa kusema, “Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikisema kwamba City wana kikosi bora, lakini hawafanyi kile kinachotakiwa na nadhani njaa ya mafanikio itarudi tena chini ya utawala wa Pep Guardiola.”

Naye Gary Neville ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Manchester United ameipa nafasi timu yake hiyo ya zamani kuchukua ubingwa huo kutokana na usajili wa wachezaji uliofanywa na kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho.

Ligi ya Uingereza ndiyo ligi inayoongoza duniani kwa kupendwa pamoja na kutazamwa na mashabiki wengi ikiwemo nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents