Burudani ya Michezo Live

Herieth Paul apata shavu kwa mara nyingine kwenye Victoria’s Secret

Mtanzania, Herieth Paul anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masula ya mitindo baada ya Ijumaa hii kupokea mualiko wa kuwa miongoni mwa warembo ambao watatembea kwenye maonyesho makubwa ya mitindo duniani, Victoria’s Secret.

Kwa sasa mrembo huyo anapata nafasi hiyo kwa mara ya tatu toka mwaka 2016 ambapo alichaguliwa kwa mara ya kwanza.

“I watched my first vs show when I was 13 years old. I am so beyond excited to be walking my third @victoriassecret fashion showI am so grateful for this opportunity,” Mrembo huyo aliandika Instagram na kuwashukuru “Thank you @johndavidpfeiffer @monica.mitro @10magazine @ed_razek1 and my amazing team @womenmanagementny @angiesmodels Ya’ll dreams do come true ❤️ #3”

Maonyesho hayo makubwa yatafanyika siku ya kesho Disemba 2 ambapo warembo mbalimbali kutoka watatembea kwenye jukwaa hilo.

https://www.instagram.com/p/Bq0mFs3gwtS/

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye duru mbalimbali za habari inadai kwamba kutembea kwenye maonyesho hayo unalipwa zaidi ya bilioni moja.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW