Habari

Hero to Zero: Baada ya kuporomoka kimuziki member wa KALAMASHAKA ya Kenya sasa anauza karanga kujipatia kipato!

Kalamashaka au K-Shaka ni kundi la hip hop kutoka Kenya lililoanzishwa katikati ya miaka ya 90 likiwa na members watatu. Hili ni kundi ambalo kwa miaka ile lilipata umaarufu mkubwa na kufanikiwa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa akiwemo Dead Prez. Pia Walifanikiwa kuperform katika nchi mbalimbali za Afrika na ulaya ikiwa ni pamoja na Nigeria, South Africa, Sweeden, Norway na kwingineko.

kalamashaka (1)

Yawezekana umeshajiuliza wasanii wa kundi hili kongwe wamepotelea wapi, kwa mujibu wa Kenyan Post, mmoja wa members wa kundi hilo sasa anauza karanga maeneo ya Umoja estate, Nairobi kwaajili ya kujipatia kipato.

Kwa mujibu wa chanzo hicho member huyo wa K-Shaka alionekana akitembeza karanga katika pubs za maeneo ya Umoja estate ambako pia inasemekana huomba omba pombe pamoja na kugongea sigara kwa watu katika club za usiku.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba member huyo inasemekana pia amekua ‘drug addict’ kitu ambacho kinazidi kumpotezea muelekeo wa maisha na muziki pia.

Kalamashaka ni kundi lililowahamasisha wasanii wengi wapya waliokuja baada yao kama Necessary Noise, K-South, Gidi gidi majimaji na wengine.

Sikiliza moja ya hit song ya Kalamashaka

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents