HabariUncategorized

HESLB yatangaza majina mapya ya awamu ya nne ya wanafunzi waliopata mikopo

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha nyingine ya awamu ya nne ya majina ya wanafunzi 1,775 wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na kufanya jumla ya idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353.

Katika Awamu ya Kwanza, Pili na ya tatu takribani wanafunzi 29, 578 wa mwaka wa kwanza walipata mikopo ya elimu ya chuo kikuu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana (Jumapili, Novemba 12, 2017) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bwana, Abdul-Razaq Badru, amesema orodha kamili ya wanafunzi hao inapatikana katika tovuti ya Bodi hiyo ingia hapa (www.heslb.go.tz) na pia imetumwa kwa vyuo husika leo ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.

Tumekua tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea, na kila tunapokamilisha, tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa mikopo ambao wana sifa – leo tumetoa hao 1,775.” amesema Bw. Badru.

Bwana Badru, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pia amekumbusha kuwa kiasi cha shilingi bilioni 427.54 zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi bilioni 147.06 kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2017/2018. Fedha hizo, shilingi bilioni 427.54, ni kwa ajili ya wanafunzi 122,623 wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo vyuoni.

Hata hivyo, Bodi ya Mikopo (HESLB) imetangaza kufungua dirisha la rufaa kuanzia leo, Jumatatu Novemba 13, 2017 hadi Novemba 19, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili.

Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote nchini kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo kabla ya Novemba 22, 2017 ili kuiwezesha Bodi kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017.” amesema Bw. Badru katika taarifa yake.

Kupata Maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufaa yako bonyeza kwenye link hapa mbele (www.heslb.go.tz).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents