Tupo Nawe

Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine kwa wapenzi walioachana (EX)

Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine kwa wapenzi walioachana (EX)

Maafisa wa kituo cha maonesho ya wanyama cha San Antonio nchini Marekani wametoa ofa kwa mwenye Dola 5 sawa na Sh. 11,550, atapewa Mende ampatie jina la mpenzi wake wa zamani (Ex) na kisha kumlisha mnyama yoyote kwenye siku ya wapendanao ‘Valentine Day’.

Mende na Ua la Valentine

Tukio hilo limepewa jina la “Cry Me a Cockroach” ikimaanisha ‘ning’ate mimi Mende’ ambapo wataruhusiwa hata wale ambao wapenzi wao wa zamani hawaishi Jijini Texas na Marekani kwa ujumla.

Cry Me A Cockroach | San Antonio Zoo

Broken Hearted This Valentine’s Day? Purchase A Cockroach Or Rat, Name It After Your Ex, And We’ll Feed Them To One Of Our Animals

Kwa wale ambao wapenzi wao wa zamani walikuwa ni wabaya zaidi kwao au wakatili, watatakiwa kulipia Dola 20 sawa na Sh. 46,206 ili kupewa panya na kuwapa majina ya wapenzi wao wa zamani kisha kuwalisha wanyama.

Hiyo itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa kituo hicho kufanya tukio la aina hiyo ambalo limezua hisia za mshangao na kuvutia kwa watu mbalimbali.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW