Michezo

Hii ndio adhabu ambayo mahakama imewapungizia Real Madrid

Klabu ya Real Madrid hatimaye imepunguziwa adhabu na mahakama ya usuluhishi ya michezo saivi wataweza kusajili wachezaji katika kipindi cha kiangazi mwaka 2017.

Mwaka huu FIFA ilitangaza kuzipiga marufuku klabu za Real Madrid na Atletico Madrid kufanya usajili kwa vipindi viwili kufuatia kuvunja taratibu na sheria za usajili wa wachezaji chini ya miaka 18 kutoka nje.

Lakini baada ya mabingwa hao wa Ulaya na dunia kukata rufaa, wamepunguziwa adhabu hiyo huku mahasimu wao Atletico Madrid wakiwa bado hawajapewa neno lolote kutoka katika mahakama hiyo, Adhabu hiyo ilikuwa ni ya vipindi viwili vya usajili vya mwaka 2017.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents