Michezo

Hii ndio bajeti ya Simba SC msimu huu ni kufuru, Mo Dewji asema anafanya hivyo kuwapa ujasiri Yanga

Mfanyabiashara maarufu barani Afrika na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo katika msimu wa 2019/20 itakuwa mara mbili na nusu ya ile msimu uliopita ambayo ilikuwa ni Tsh. Bilioni 1.3 .

Akiongea na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Mo Dewji amesema kuwa ameongeza bajeti hiyo ili kuifanya iwe klabu bora na kubwa zaidi barani Afrika.yenye kushindana na vilabu vikubwa barani Afrika.

Mwaka uliopita tulitumia kama dola milioni $1 hivi, Tukanunua wachezaji wakubwa wa Kimataifa, tukatengeneza mfumo wa kusaka wachezaji ‘Scouting’ pamoja na kumpata kocha mkubwa. Bajeti yetu ya msimu uliopita itakuwa ndogo kama mara mbilina nusu hivi ukilinganisha na ya msimu huu.” amesema Mo Dewji.

Akielezea sababu za uwekezaji mkubwa ndani ya klabu ya Simba, Mo Dewji amesema kuwa lengo lake kubwa ni kuhamasisha pia mashabiki kupenda timu za nyumbani zaidi kuliko zile za Ulaya.

Unajua miaka mitano iliyopita mashabiki wa mpira walikuwa wanaingia watu 500 uwanjani, Watu walipoteza kabisa hamasa ya mpira. Ukiangalia kwa mwongo mmoja uliopita watu wengi walikuwa wanafuatilia vilabu vya Ulaya kama Liverpool,, Man United Arsenal.. Mpira wetu haukuwa na mvuto, Hakuna mtu aliyejali habari za Simba.“amesema Mo Dewji.

Mo Dewji amesema pia uwekezaji wake hautaisaidia Simba SC peke yake bali hata vilabu vingine kwani utawapa hamasa, “Ninaamini Simba haiwajengi tu wapinzani, pia inazipa ujasiri timu zingine, ukiwa na timu nzuri za ndani pia unakuwa na timu nzuri ya Taifa na hapo ndio wachezaji wataweza kwenda kucheza Ulaya na sehemu nyingine“.

Kuhusu mitandao ya kijamii, Mo Dewji amesema kuwa alitumia fursa ya kukuza kurasa za mitandao ya kijamii za klabu ya Simba kuwa za kiweledi zaidi ikiwa ni pamoja na kuzi-verify baada ya kuona Watanzania wengi wanafuatilia mitandao ya kijamii.

Msimu uliopita, Simba SC walitumia Tsh. Bilioni 1.3 kwa hiyo kwa makadirio ya msimu huu huenda wakatumia zaidi ya Tsh. Bilioni 3.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents