Michezo

Hii ndio kauli ya Manchester City baada ya kufungiwa kushiriki UEFA kwa misimu miwili kwa makosa haya

Hii ndio kauli ya Manchester City baada ya kufungiwa kushiriki UEFA kwa misimu miwili kwa makosa haya

Manchester City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana kwamba wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni.

Mabingwa hao wa ligi ya Premier pia wamepigwa faini ya euros milioni 30 (£25m). Hata hivyo umauzi huo unaweza kupigwa katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo. Manchester City imesema kwamba hatua hiyo ni jambo la kukatisha tamaa lakini wala halikuwashangaza na watakata rufaa.

Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye mahesabu yake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ilionesha kwamba hawakupata hasara wala faida”, na kuongeza kwamba klabu hiyo haikutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi”.

Imesemekana kwamba City huenda pia ikapunguziwa pointi katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja. Hata hivyo, adhabu hiyo haitakuwa na athari zozote kwa timu ya wanawake ya City.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manchester City: “Klabu hiyo imekuwa ikifikiria umuhimu wa kuwa na bodi huru na kufuatwa kwa mchakato usiopendelea upande wowote kuangalia ushahidi wao ulio wazi.

“Desemba 2018, mchunguzi mkuu wa Uefa alisema wazi vikwazo ambavyo anataka City iwekewe hata kabla ya uchunguzi kuanza kufanywa.

“Kasoro na udhaifu uliopo katika mchakato wa Uefa kwenye uchunguzi alioongoza, hakukuwa na shaka na matokeo ya uchunguzi huu. Klabu hii awali ilikuwa imewasilisha malalamiko yake kwa bodi ya nidhamu ya Uefa, ambayo yaliidhinishwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.

“kwa maneno rahisi, hii ni kesi iliyowasilishwa na Uefa, ikashtakiwa na Uefa na aliyetoa uamuzi ni Uefa. Kwa mchakato wa kibaguzi aina hii ambao umemalizika, klabu hii sasa itatafuta hukumu isiyopendelea upande wowote haraka iwezekanavyo na hivyo basi, kwanza kabisa itaendelea na mchakato wake katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo bila kuchelewa.”

City imepangwa kucheza na Real Madrid katika timu 16 za mchujo za ligi ya mabingwa huku mchuano wa kwanza ukiwa ni Februari 16 katika uwanja wa Bernabeu.

Rais wa La Liga Javier Tebas iliisifu Uefa kwa kuchukua hatua stahiki.

“Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa fedha na kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria hiyo ni jambo la msingi kwa hatma ya mpira wa kandanda,” amesema.

“kwa miaka mingi tumekuwa tukitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua muafaka dhidi ya Manchester City na Paris Saint-Germain, na hatimaye tumepata mfano bora na ni matumaini yetu kwamba hili litaendelezwa. Ni kheri kuchelewa kuliko kutochukuliwa kwa hatua kabisa.”

line

Uchambuzi – je uamuzi huu utamaanisha nini kwa Guardiola?

Na Simon Stone, mwanahabari wa BBC Michezo

Hizi ni taarifa nzito. Ukiangalia walivyotoa taarifa kwa haraka kujibu uamuzi huo, unaweza kutathmini kwamba walikuwa wamejianda lakini pengine hawakutarajia uzito wa uamuzi uliochukuliwa.

City imesema wazi na hata katika mazungumzo ya kibinafsi kwamba inapanga kupinga uamuzi huo. Bado inang’ng’ania kuwa na jopo huru – kwasababu kwa mtazamo wao hawaoni kama bodi iliyochukua uamuzi huo ilifikia viwango hivyo.

Hata hivyo, hadi kufikia sasa, klabu hiyo imeondolewa katika ligi ya mabingwa Ulaya kwa misimi miwili, na kuzua maswali mengi.

Pep Guardiola kila wakati amekuwa akisema kwamba atasalia City hadi kandarasi yake itakapomalizika 2021 lakini pia amesema kwamba anaamini uongozi wa klabu wanapomuambia kwamba hakuna kosa walilofanya.

Iwapo watachukua ubingwa msimu huu katika ligi ya mabingwa au la, je Guardiola ataamua kuondoka? Na iwapo atafanya hivyo, vipi kuhusu hatma ya wachezaji nyota wa klabu hiyo ambao wengi wao walijiunga na klabu hiyo kwasababu yeye alikuwa meneja.

Ni bila shaka ni hali ya kusisimua na ni wazi kwamba bado ufumbuzi wa suala hili uko mbali kupatikana.

line

Nini ambacho City inadaiwa kufanya?

Uefa ilianzisha uchunguzi baada ya gazeti la Ujerumani Der Spiegel kuchapisha nyaraka za siri zilizovuja Novemba 2018 zilizodai kwamba City iliweka kiwango kikubwa cha makubaliano ya ufadhili wao na kupotosha bodi ya soka ya Ulaya.

Taarifa hiyo ilidai kwamba City – ambayo kila wakati imekuwa ikikanusha kufanya makosa – ilipotosha Uefa kwa kukusudia ili iweze kutimiza sheria ya FFP inayotaka vilabu kufikia kiwango cha fedha ambacho siyo kuwa na hasara wala faida. City ilipigwa faini ya £ milioni 49 mwaka 2014 kwasababu ya kosa la awali la kukiuka sheria.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents